• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi afungua semina ya ufuatiliaji na udhibiti wa matumizi ya dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya.

Imerushwa: September 18th, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen amefungua semina ya ya ufuatiliaji na udhibiti wa matumizi ya dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya na namna ya uagizaji wa dawa kutoka Bohari kuu ya dawa.

Bw. Stephen amempongeza  na kumshukuru Mhe  Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiona sekta ya  afya kwa unyeti wake na kuamua kutoa kiasi cha Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Sindeni kwenye  Halmashauri yetu ya Handeni.

Pia Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza sekta ya Afya kwa utendaji wao wa kazi lakini amewakumbusha kufanya kazi kwa bidii na kila mmoja aipende kazi yake na atimize majukumu ya kwenye idara. Semina hii imekuja Handeni kwakuwa kuna watu hawatimizi wajibu wao ndiyo maana wawezeshaji wamekuja kuwakumbusha ili mtimize wajibu wenu.Ameeleza.

Ameongezea kusema kuwa kama Halmshauri hatuwezi kutumia fedha kwaajili ya kutoa elimu kwa watu ambao tayari wameshasomea ujuzi huo yatuapasa kutumia lasilimali fedha kwaajili ya kutolea huduma kwa jamii. Lengo la semina hii ni kupata matokeo chanya ya mapato na upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma.

Kwa kumalizia Bw. Saitoti Z. Stephen  amewaongoza timu ya usimamaizi ya afya  kuweka maazimio ambayo yatawaongoza kusimaia na kuleta ufanisi wa kazi kwenye utendaji wa kazi.Maazimio hayo ni

1: Timu ya usimamizi wa afya kupitia taarifa ya uagizaji dawa.

2: Ujazaji wa fomu za bima ya afya ufanyike kikamilifu na kwa usahihi na kuata mrejesho wa fedha zilizokatwa.

3: Taarifa za uagizaji dawa kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma, zifike kwa mfamasia kabla ya tarehe nne ya kila mwezi.

Nao wawezeshaji wa semina hii wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni kwa kuamua kuweka utaratibu wa kila mkuu wa idara kuwa mlezi wa kata ili kurahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya kata pamoja na swala zima la afya kwa kila kata kwa ukaribu zaidi.

Kwa upande wa kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt.  William Awe amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuandaa semina hii ili kuwakumbusha wataalam majukumu yao ili walete matokeo chanya ya mapato na upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya. Na swala la msamaha tumepata elimu ya kutosha kuahidi kuyafanyia kazi.

Afisa ustawi wa Jamii Ndugu Jovin John ameeleza kuwa kundi la watu maalum ndiyo wanaopaswa kupewa msamaha na sio kila mtu, ameyataja makundi hayo ni pamoja na watu wanaopata ajali wanaenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa na fomu ya polisi namba tatu, wazee wasiojiweza, watoto chini ya miaka mitano wakiwa na kadi za kliniki pamoja na wamama wajawazito hivyo amewakumbusha wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya wanapotoa msamaha waangalie kundi hilo lenye uhitaji kulingana na miongozo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Z. Stephen akiongea wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo.

Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. William Awe akitoa ufafanuzi kwenye kikoa hiko

Ndugu Vendavenda Sumuni ambaye ni katibu wa Afya akisikiliza kwa umakini maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri.

Afisa Ustawi wa Jamii Ndugu Jovin John aliyesimama akitoa ufafanuzi kwenye kikao hicho.

Baadhi wa wshiriki wa semina hiyo.

Wataalam wa Idara ya Afya wakiwa makini kuwasikiliza wawezeshaji wa Semina hiyo.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HANDENI DC June 04, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa