Baraza la madiwani linalounda Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa pamoja limepitisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Halmashauri imekasimia kuwa na kiasi cha Tsh.49,787,608,984/=, ikiwa ni ongezeko kutoka Tsh.38,872,491,064/= kwa mwaka 2017/2018.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekasimia kukusanya mapato ya ndani kiasi cha Tsh.2,196,374,052/=, Matumizi ya kawaida Tsh.2,009,206,000/=, Bajeti ya miradi ya maendeleo inatarajiwa kuwa na jumla ya Tsh.5,838,831,132/= na Mishahara inakisiwa kuwa na jumla ya Tsh.39,743,197,800/=.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh.Ramadhani Diliwa amesisitiza ukusanyaji wa mapato ya ndani huku akieleza kuwa, ruzuku kutoka Serikali kuu hazifiki kwa wakati na Kwa asilimia iliyoombwa kutokana na Serikali kuwa na miradi mingi ambayo ni mikubwa inayotekelezwa kwa manufaa ya Nchi.
Ameitaka ofisi ya Mkurugenzi na timu ya mapato kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi katika kuhakikisha vifungu vilivyotengwa vinakusanywa vizuri huku akisisitiza usimamizi wa urejeshwaji wa vitabu vya mapato kwa wakati ili kuepuka ubadhilifu fedha.
Aidha amewaomba Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanaendeleza umoja wa kushiriki kwenye suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwasababu manufaa ya kukusanya mapato pasipo kutumia mawakala yameonekana tayari kwamwaka wa fedha 2017/2018, hivyo washiriki kikamilifu ili kutimiza malengo ya Halmashuri.
Baraza la madiwani la kupitia na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 limefanyika kwa sikumbili kuanzia tarehe 16-17/01/2017.
LikeShow More ReactionsCommentShare
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa