NI Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tangu Julai.2016 ambapo ni mara ya kwanza kwake kuwa Mkurugenzi baada ya Kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutumikia wananchi wa Wilaya ya Handeni. Kabla ya kuwa Mkurugenzi Bw. William Makufwe alikuwa Afisa Mipango Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa muda wa miaka 10.Anataaluma ya mipango na bajeti, kufanya tafiti mbalimbali na pia ni mtaalamu wa mambo ya programu, mipango na menejimenti.
MALENGO YAKE KWA HALMASHURI YA WILAYA YA HANDENI.
1. Kusimamia na kuboresha mifumo ya utendaji kazi kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji kuanzia ngazi ya Vitongoji hadi Halmasuri.
2. Kusimamia watendaji na kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi kwa kuwasikiliza na kutatua kero zao kuanzia ngazi ya Vitongoji.
3. Kusimamia rasilimali za Halmashauri na Serikali kwa kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya wananchi tu.
4. Kufanya ushawishi kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili waweze kusaidia Halmashauri katika maendeleo kwa nyanja mbalimbali.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa