MAJUKUMU YA IDARA
Maendeleo ya Jamii
1.Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
2.Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
3.Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
4.Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbali mbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
5.Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
6.Kueneza elimu ya Uraia mwema.
7.Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
8.Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
9.Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
10.Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
11.Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
12.Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
13.Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
14.Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
USTAWI WA JAMII
1. Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo, Kanuni na viwango vya ubora katika utoaji wa huduma mbalimbali za ustawi wa jamii.
2. Kufanya tathmini, ufuatiliaji na utaratibu wa huduma za ustawi wa jamii.
3. Kufanya tafiti zinazohusu huduma za ustawi wa jamii.
4. Kuwajengea uwezo watumishi wa ustawi wa jamii na Wadau katika utoaji wa huduma.
5. Kuanzisha na kuendeleza programu za kushawishi, kutetea na kulinda haki za makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu wa viungo na ngozi, wazee na wasiojiweza, familia zenye dhiki na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
6. Kujenga Uhusiano na wadau wa nje na ndani ili kutoa huduma bora za ustawi wa jamii.
Maendeleo ya Vijana
1.Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana.
2.Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya vijana.
3.Kuhamasisha vijana kufufua moyo wa kujitolea kwa ajili ya Maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
4.Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya uzazi na kujamiina kwa Vijana.
5.Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, ajira kwa vijana na elimu ya familia kwa kushirikiana na Vyama visivyo vya kiserikali.
6.Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu vijana.
7.Kuratibu shughuli za NGOs mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Vijana.
8. Kuandaa mpango wa kuboresha malezi ya vijana.
9.Kuhamasisha waajiri na wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa vijana katika maeneo mbalimbali.
10.Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo vijana ili kuwawezesha kujiajiri.
11.Kuandaa mipango ya kuhamasisha vijana ili kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiajiri.
12 Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
13.Kuandaa na kuratibu shughuli za matamasha ya vijana.
14. Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs na CBOs zinazofanywa ngazi ya Wilaya.
15.Kuratibu mafunzo ya utoaji wa mbinu za kuwasaidia vijana kujikomboa na umaskini, ujinga, kupiga vita UKIMWI, madawa ya kulevya na kutetea usawa wa jinsia.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa