IDARA YA UJENZI
Idara ya ujenzi ni mojawapo ya idara kuu zinazounda Halmashauri ya wilaya ya Handeni. Idara ya Ujenzi ni Idara iliyoundwa katika mamlaka ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) kwa madhumuni ya
1. Kusimamia na kutengeneza barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,
2. Kusimamia Ujenzi wa majengo ya Serikali na kutoa ushauri wa namna iliyobora ya ujenzi huo; pia miradi ya Mashirika yasio ya ki – Serikali pamoja
3. kutoa ushauri wa ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi ,
4. Kusimamia matengenezo ya magari, mitambo na nishati ya umeme kwenye majengo ya Serikali katika Halmashauri ya wilaya.
MUUNDO WA IDARA YA UJENZI
VITENGO VYA IDARA YA UJENZI
IdarayaUjenziimeundwanavitengovifuatavyo:
1. Kitengo cha Barabara
2. Kitengo cha Majengo
3. Kitengo cha Magarinamitambo
4. Kitengo cha Umeme
WATUMISHI WA IDARA YA UJENZI.
Idara ya Ujenzi inaundwa na watumishi wa fuatao kwasasa:
1. Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Handeni (District Engineer) - mmoja
2. Watumishi wenye taaluma ya uhandisi (Engineers) - wawili
i) Barabara (Civil works mmoja)
ii) Majengo (Building mmoja)
3. Watumishi wenye taaluma ya fundi sanifu(Technicians)
i) Barabara (Civil works) - mmoja
ii) Majengo (Buildings) - wawili
iii) Magari (Mechanical) -mmoja
iv) Seremala (Carpenter) -mmoja
v) Fundi ujenzi (masonry) - mmoja
4. Watumishi wenye taaluma ya udereva
i) Dereva -mmoja
BARABARA
MTANDAO WA BARABARA
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inamtandao wa barabara wenye jumla ya urefuwa Km 820 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo:
- Km 91 ni barabara kuu (kitaifa) ni zalami na zinahudumiwa na TANROADS
- Km 166 ni barabara za Mkoa (km 111 lamina km 55 changarawe) hizipia zinahudumiwa na wakala wa barabara TANROADS
- Na km 563 ni barabara za wilaya na vijiji ambazo zinahudumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
HALI YA BARABARA KWA UJUMLA
Barabara zote za wilaya na vijijini ni za udongo na changarawe kidogo. Hali ya barabara kwa kiasi kikubwa ni ya wastani kwani baadhi ya barabara hujifunga kwa muda wakati wa mvua, hasa maeneo korofi, pia baadhi bado hazijaimarishwa kiasi cha kuweza kubeba magari mazito wakati wa mvua.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kupitia Idara ya ujenzi huzifanyia matengenezo barabara za Halmashauri na vijiji kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara kama ifuatavyo:-
i) Matengenezo ya kawaida (Routine maintenance works)
ii) Matengenezo ya sehemu korofi (Spot improvement works)
iii) Matengenezo ya muda maalumu (Periodic maintenance works)
iv) Ukarabati wa madaraja na makalvati(Bridges and culvert maintenance)
MAFANIKIO
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kupitia Idara ya Ujenzi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukarabati/kufungua barabara kutoka makao makuu ya Wilaya hadi makao makuu ya Vijiji vya Halmashauri kwaajili ya kuboresha huduma katika sekta ya usafiri na usafirishaji. Jumla ya km 156 zimewekwa kifusi na zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
MAJENGO.
Idara ya Ujenzi husimamia ukarabati na ujenzi wa majengombalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kamaifuatavyo:
- Nyumba za waganga, zahanati na vituo vya afya
- Nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari
- Ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari
- Ujenzi/Ukarabati wa Ofisi za Idara mbalimbali za Halmashauri
Pia idara hutoa ushauri wa namnailiyo bora ya ujenzi wa majengo katika miradi ya Mashirika yasio ya ki – Serikali pamoja na kutoaushauri waujenzi wa nyumba bora kwa wananchi.
MAGARI NA MITAMBO.
Idara ya Ujenzi huyafanyia matengenezo madogomadogo magari na mitambo ya serikali katika karakana yake iliyopo ujenzi, pia huratibu na kukagua magari yote ya Halmashauri kwaajili ya matengenezo mbalimbali kupitia mtaalamu wa magari wa Idara. Magari yote ya Halmashauri hukaguliwa kwanza na mtaalamu wa magari wa idara kabla ya kupelekwa kwa wazabuni kwaajili ya matengenezo makubwa.
UMEME
Idara ya ujenzi pia kuna kitengo cha umeme.Kitengo hiki kupitia mtaalamu wa idara hufanya shughuli za ukarabati na uwekaji wa mfumo wa Umeme katika majengo yote ya Halmashauri na serikali yaliyopo hapa wilayani.
wa mfumo wa Umeme katika majengo yote ya Halmashauri na serikali yaliyopo hapa wilayani.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa