Kuratibu shughuli zote zihusuzo uchaguzi(uchaguzi wa serikali za Vijiji, uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo zote zitakazo jitokeza baada ya uchaguzi kufanyika).
Kuratibu mazoezi yote ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa uchaguzi mkuu na Orodha ya wapiga kura kwa Uchaguzi wa serikali za Vijiji.
Kuratibu maswala yote muhimu kwa ajili ya kuwezesha mazoezi ya uchaguzi (maswala hayo ni pamoja na maandalizi ya uteuzi wa wagombea, kuratibu kampeni za wagombea, maadalizi ya vituo vya kupigia kura, mafunzo kwa washiriki wote wa mazoezi ya uchaguzi. Mambo yote haya yanafanyika kwa ushiriki wa karibu na TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na Wizara inayosimamia Uchaguzi wa serikali za Vijiji).
Kushirikiana na Idara ya Utumishi kuhakikisha mafunzo ya mara kwa mara yanafanyika kwa Wenyeviti wa Serikali zaVijiji ili kuwawezesha kutekeleza majukum yao kwa Mujibu wa Sheria.
Kumshauri Mkurugenzi juu ya maswala yote yahusuyo uchaguzi katika Halmashauri ili kuwezesha mazoezi hayo kufanyika kwa mujibu wa Sheria.
Kutekeleza majukum mengineyo kwa maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri.