MAJUKUMU YA IDARA YA MAZINGIRA NA UDHIBITI WA TAKA NGUMU
1. Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana na usimamizi wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
2. Kufuatilia na kuainisha maeneo yaliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambayo yanayopaswa kuhifadhiwa.
3. Kushiriki katika kuandaa Mpangokazi na Bajeti ya Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu ya kila mwaka.
4. Kushiriki kuutekeleza Mpango kazi wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu.
5. Kutoa Elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa Jamii na wadau wengine.
6. Kukusanya Takwimu na Taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi na hifadhi ya Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
7. Kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirka kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (Kama vile – Uchimbaji wa madini,Kilimo, Ujenzi, Ufugaji nk.)
8. Kushiriki katika kupanga na kusimamia zoezi zima la Usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi.
9. Kupitia Taarifa za Tathmini ya athari kwa Mazingira (EIA) zilizopo katika makampuni na Taasisi mbali mbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kuzifanyia kazi.
10. Kuandika Taarifa ya kazi ulizozifanya katika mwezi husika na kuiwasilisha Taarifa hiyo kwa Afisa Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu (H/W).
11. Kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauriya Wilaya ya Handeni.
12. Kujaza Fomu ya wazi ya mapitio na upimaji wa utendaji wa kazi (OPRAS) kwa kila mwaka.
13. Kufanya kazi nyinginezo utakazopangiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa