TARATIBU ZA KUFUATA ILI KUSAJILI KIKUNDI CHA SANAA
1. KIKUNDI KIWE NA KATIBA NA MUHTASARI WA KIKUNDI CHAO.
2. KUIPELEKA OFISI YA UTAMADUNI YA WILAYA KWA UKAGUZI.
3. KUCHUKUA FOMU YA USAJILI OFISI YA UTAMADUNI WILAYA
4. KIKUNDI KINAANDAA MALIPO YA KIASI CHA SHILINGI ELFU SABINI NA
TANO(75000) AMBAPO ASILIMIA 25 INALIPWA HALMASHAURI SAWA NA
18750 NA ASILIMIA 75 INALIPWA BASATA SAWA NA 56250.
KUJISALI MTU BINAFSI
1. ANDAA ANDIKO LA KWANINI UNATAKA KUANZA KAZI HUSIKA YA
SANAA.
2. KUIPELEKA OFISI YA UTAMADUNI YA WILAYA KWA UKAGUZI.
3. KUCHUKUA FOMU YA USAJILI OFISI YA UTAMADUNI WILAYA
4. KUANDAA MALIPO YA KIASI CHA SHILINGI ELFU SABINI NA TANO
(75000) AMBAPONASILIMIA 25 INALIPWA HALMASHAURI SAWA NA
18750 NA ASILIMIA 75 INALIPWA BASATA SAWA NA 56250.
KUSAJILI STUDIO
1. ANDIKA KATIBA NAKALA TATU
2. WASIFU WA MSIMAMIZI WA STUDIO HUSIKA.
3. TIN NAMBA.
4. CHUKUA FOMU YA USAJILI OFISI YA UTAMADUNI WILAYA AU
PAKUA KWENYE MTANDAO.
5. GHARAMA ZA USAJILI NI 250,000 AMBAPO ASILIMIA 25 INAENDA
HALMASHAURI NA 75 INAENDA BASATA.
KUFANYA MALIPO YA USAJILI.
1. KWENDA KWA MHASIBU KUCHUKUA KIBALI CHA KULIPIA BENKI.
2. KURUDISHA HATI YA MALIPO KWA MHASIBU TENA KWAAJILI YA KUPATA
RISITI YA MALIPO YA ASILIMIA 25.
3. KWENDA NA RISITI BARAZA KUMALIZIA USAJILI.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa