• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Handeni wafanya Msaragambo

Imerushwa: December 29th, 2018

Uongozi wa Wilaya ya Handeni umeungana na wananchi kufanya msaragambo wa kuchimba msingi wa madarasa matano shule ya Sekondari Kwaludege iliyoko Kata ya Kabuku Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga leo tarehe 29-12-2018 lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaendelea na masomo ya Sekondari bila kukwamishwa na uhaba wa madarasa.

Akizungumza katika amsha ari hiyo kwa wananchi ili kutoa nguvu kazi ya kujenga madarasa hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alisema wananchi wawe wazalendo kwa kujitolea kazi za maendeleo ikiwepo kujenga madarasa kwani elimu ni urithi pekee ambao mtu anaweza kumpatia mtoto

Aidha amewaomba wadau wa elimu kutoka maeneo mbalimbali wajitokeze kuchangia ujenzi huu wa madarasa ili kukamilisha madarasa hayo  haraka na wanafunzi waweze kupata nafasi ya kusoma hasa wale amabao hawakuchaguliwa awamu ya kwanza.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William  Makufwe alisema Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inauhaba wa madarasa 49 ambapo itagharimu kiasi cha zaidi ya sh.500,000,000 (million mia tano) kwa mahitaji ya mabati, matofali, saruji, misumari, mbao, nondo, kokoto, chokaa, mchanga  hivyo anawaomba wadau wa elimu ndani na nje ya Handeni wachangie chochote kupitia  akaunti ya mfuko wa elimu namba 4141200084 benki ya NMB au wanaweza kuchangia kupitia namba zifuatazo 0754832436 au 0712018833 au 0784387557 ili kukamilisha madara hayo mapema na wanafunzi waanze masomo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni Bw. Athumani Malunda amewataka viongozi wa Kata hiyo kuwajibika ipasavyo kukamilisha kazi hiyo ya ujenzi wa madarasa  mapema ili wanafunzi wasipate shida na kwamba wasiruhusu siasa isiingilie masuala ya maendeleo.

Pia amewataka wawekezaji walioko Handeni wahakikishe wanachangia shughuli za maendeleo la sivyo hakuna sababu ya wawekezaji hao kuwepo Handeni kama hawatachangia  maendeleo ya Handeni.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Mwl. Boniphace Maiga aliwapongeza wananchi kujitokeza katika shughuli hiyo ya uchimbaji wa msingi huo na kuwataka wananchi hao kuendelea na moyo huo mpaka madarasa hayo yatakapokamilika na kwamba serikali iko tayari kuungana na wananchi kutatua tatizo la uhaba wa madara.

Aidha ametoa onyo kwa wale ambao wanawapa wanafunzi mimba kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watu hao pamoja na mzazi na mtoto aliyepewa ujauzito(Serikali itawaonyesha namna bora watu hao)alisema.

Wananchi wa Kata ya Kabuku kwa pamoja walipongeza juhudi za viongozi wa Wilaya na wameahidi kujitolea hadi ujenzi huo utakapokamilika na wamesema wao hawako tayari kuona watoto wanabaki nyumbani kutokana na uhaba wa madarasa.

MWISHO.


Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akichimba msingi

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akichimba msingi.


Katibu Tawala Mwl.Boniphace Maiga akishiriki kikamilifu katika Msaragambo huo







Wadau mbalimbali walijitokeza kuhakikisha misingi ya madarasa matano yamekamilika

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa