• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WA MKATA KUTUMIA FURSA YA KUPATA MIKOPO BAADA YA UZINDUZI WA TAWI JIPYA LA NMB BENKI

Imerushwa: November 14th, 2017

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigella leo amezindua rasmi tawi la NMB benki lililopo Kata ya Mkata Wilayani Handeni na kuwataka wakazi wa maeneo ya jirani kuacha kuhifadhi fedha nyumbani.

 Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ufunguzi wa tawi hilo la kibenki ni fursa kubwa kwa wakazi wa Mkata na maeneo ya jirani kwani huduma za kifedha zimesogezwa karibu na  ni chachu ya ukuaji wa maendeleo na uchumi wa Mkata.


 Aliongeza kuwa Mkata ni eneo lenye mzunguko mkubwa wa kifedha kutokana na kuwa na wafanyabiashara mbalimbali, wakulima, wafugaji,wafanyabiashara wa matunda na biashara nyingine hivyo wanategemea kwa kiasi kikubwa huduma ya benki katika utunzaji wa fedha  na usalama wao.

 Mh. Shigella  alisema kuwa NMB Benki imesaidia sana wananchi kwa kutoa mikopo  na misaaada mingine ya kijamii hivyo ni vyema kuitumia benki hiyo kwani kwa kufanya biashara na NMB ni kufanya biashara na serikali kwa sababu kwa upande mwingine NMB ni Serikali ambapo  fedha zinazowekwa ndizo zinazorudi kwenye jamii kwa mtindo wa mishahara, ujenzi wa miundo mbinu na huduma nyingine za kijamii.

 ”wananchi  muweke utaratibu wa kuhifadhi fedha zenu kwenye benki badala ya kuzikumbatia ndani hali inayopelekea kuhatarisha usalma wa maisha yenu, NMB imefungua tawi kuwapunguzia kufuata huduma za benki mbali,  tumieni fursa hii kupata mikopo ili kukuza uchumi wenu na Taifa kwa ujumla” Alisema Mkuu wa Mkoa.

 Aidha amewataka NMB Benki kujiandaa na fursa za miradi mikubwa ya Bomba la mafuta,Viwanda,Madini, Kilimo na Ufugaji iliyopo  Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga  ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi wote kwa kuongeza matawi  mengi ili  kuepusha wananachi kuzunguka na fedha mifukoni.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ameshukuru uongozi wa NMB kwa kuona umuhimu wa kufungua tawi eneo la Mkata ambalo litawasaidia wakazi wa eneo hilo na jirani kutotembea urefu wa KM54 kufuata huduma za benki kwa kuzingatia kwamba eneo la Mkata linawafanayabiashara wengi na mzunguko wa fedha ni mkubwa.

 Wakati huohuo Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bw.Salie Mlai  ameahidi kuwa Benki yao itatoa msaada wa vifaa vya afya kwenye kituo cha afya cha Mkata vyenye thamani ya Milioni 10  ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida waliyoipata kwa jamii wanayoihudumia.

 Benki ya NMB yenye kauli mbiu ya “Karibu Yako” yenye maana ya kuweka ukaribu wa huduma za fedha kwa wananchi na kutoa bidhaa inayoendana na mahitaji ya maeneo husika ili iweze kuwa karibu,rahisi na yenye mafanikio katika mambo ya ujenzi wa Taifa.

 NMB Benki imesambaa nchi nzima kwa asilimia 97 ambapo ina ATM zaidi ya 800, Matawi 213 na mawakala 4500 ambao wanarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha.Mikopo ya wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa inatolewa ikiwa ni pamoja na  kutoa mikopo kuendana na aina ya mradi mfano Mikopo ya pembejeo za kilimo kwa wakulima.


Image may contain: 8 people, outdoor

Image may contain: 13 people, people smiling, people standing

Image may contain: 17 people, people smiling, people standing

  Image may contain: 1 person, sitting and outdoor






Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa