• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WILAYANI HANDENI WAPIGWA MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU NDANI YA MITA 60 KUTOKA VYANZO VYA MAJI.

Imerushwa: June 6th, 2017

Wananchi wilayani Handeni wapigwa marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji na kutakiwa kutunza mazingira ili kuwezesha uendelevu wa maisha.

Marufuku hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika ngazi ya wilaya katika Kata ya Mkata katika bwawa la Tulafimbo.

Gondwe alisema kuwa wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji  ndani ya mita 60. “Kwa kuzingatia sheria hiyo, kupiga marufuku kwa wananchi kufanya shughuli zozote za kibinadamu zenye kuhatarisha usalama wa maji na uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji wilayani Handeni” alisema Gondwe.

Aidha, aliwataka maafisa Tarafa, maafisa watendaji wa Kata na wenyeviti wa Vijiji  kuhakikisha wanatengeneza mipaka  kwenye maeneo ya vyanzo vya maji vyote vilivyopo Wilayani Handeni msimu huu ambao mvua imenyesha ya kutosha na vyanzo vingi vimejaa maji. “Hii itasaidia kuzuia uvamizi wa maeneo hayo na kurahisisha kuchukua hatua kwa watu watakaokwenda kinyume na amri hiyo” alisema Gondwe.

Gondwe, aliwataka wananchi wote walionunua mashamba kwa lengo la kilimo kusafisha mashamba yao kwa kuacha asilimia 30 ya uoto wa asili badala ya kusafisha maeneo yote ambayo wamenunua. “Tusipotunza mazingira, itakuwa ni ubinafsi kwa kizazi chetu na kizazi kijacho. Tukitendee haki kizazi hiki na kijacho kwa kuondoa ubinafsi wa kuharibu mazingira” alisema Gondwe.

Wakati huohuo, aliwataka viongozi ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji kutunza kutunza mazingira kwa kusimamia uwiano wa ardhi uliyopo na idadi ya mifugo ili kutunza mazingira kwa kuwa na mifugo inayoendana na rasilimali ardhi iliyopo. Aliwataka kuweka mikakati ya   kupiga chapa mifugo ili kurahisisha utambuzi wa mifugo hiyo wilayani Handeni.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe aliwataka wananchi kutunza rasilimali maji kidogo inayopatikana kwa kipindi cha mvua kwa kupanda miti kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji. Alisema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia changamoto ya upatikanaji maji ya kudumu Wilayani Handeni.

Aliwataka wakuu wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza hadi la saba na kidato cha kwanza hadi cha nne anakuwa na mti wake anaoutunza ili anapomaliza shule akikabidhiwa cheti na yeye akabidhi mti alioutunza kwa kipindi chote alichokuwa shuleni.

Maadhimisho ya wiki ya mazingira kiwilaya yalitanguliwa na upandaji miti 28,954 yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “hifadhi ya mazingira muhimili kwa Tanzania ya viwanda”.

Mwenyekiti wa Hlmashauri na Mkurugenzi mtendaji wakipanda mti.Mkurugenzi Mtendaji akisawazisha shimo la mti

Mwenyekiti wa Halmashauri Ramadhani Diliwa akizungumza na wananchi

Mkurugenzi Mtendaji William Makufwe akizungumza na wananchi

viongozi wakimpongeza mwanafunzi Miriam kwa kuwakumbusha wananchi kauli mbiu ya kiwilaya ya Mti wangu niutunze unitunze.

wananfunzi wa Sekondari Mazingara wakisherehesha wakati wa maadhimisho hayo.


wananfunzi shule ya msingi Mkata wakisherehesha kwa kutoa ujumbe ulipo kwenye bango wa "HIFADHI MAZINGIRA KWA MUHIMILI WA TANZANIA YA VIWANDA"

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa