Nugu Saitoti Zelothe Stepheni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tangu August. 2021 ambapo ni mara ya kwanza kwake kuwa Mkurugenzi baada ya Kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutumikia wananchi wa Wilaya ya Handeni. Kabla ya kuwa Mkurugenzi Bw.Saitoti Zelothe Stephen alikuwa Katibu tawala wilaya ya Mbeya.
MALENGO YAKE KWA HALMASHURI YA WILAYA YA HANDENI.
1. Kusimamia na kuboresha mifumo ya utendaji kazi kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji kuanzia ngazi ya Vitongoji hadi Halmasuri.
2. Kusimamia watendaji na kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi kwa kuwasikiliza na kutatua kero zao kuanzia ngazi ya Vitongoji.
3. Kusimamia rasilimali za Halmashauri na Serikali kwa kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya wananchi tu
.4. Kufanya ushawishi kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili waweze kusaidia Halmashauri katika maendeleo kwa nyanja mbalimbali.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa