• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Asasi ya kiraia (HOPE FOR YOUNG GIRLS) yatoa vifaa vya zaidi ya milioni nne Handeni

Imerushwa: December 20th, 2019


Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni nne vilitolewa jana Kituo cha afya cha Mkata vikiwepo  taulo za kike, mzani ya kupimia uzito wa mtoto aliyezaliwa, kanga, vifaa vya kumsaidia mama wakati wa kujifungua, mipira ya vitanda vya kina mama kujifungulia na mashuka lengo likiwa ni kuwasaidia vijana wa kike walioko shuleni na akina mama wanaopitia katika changamoto hasa wakati wa kujifungua.

Akizungumza katika mapokezi ya vifaa hivyo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bi Upendo Magashi alitoa shukrani kwa Asasi hiyo kwa kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ndoto zake na amesema tangu asasi hiyo imeanza kufanya kazi Handeni imetoa elimu kwa wanafunzi wa kike ambayo imeleta matokeo chanya. Kwa upende wa Kituo cha Afya amesema Serikali imetoa zaidi ya Milioni mia nne kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya vituo vya afya pamoja na vifaa tiba hivyo amewashukuru kuunga mkono juhudi hiyo pia.

Bi.Upendo pia alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kushirikiana ili kuhahakikisha mtoto wa kike anafikia ndoto zake lakini pia aliwataka Maafisa elimu kuhakikisha wanachagua walimu ambao wanafunzi wanaweza kupeleka matatizo yao na kwamba majina ya walimu hao yapelekwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili waweze kufanya ufuatiliaji.

Alihitimisha kwa kumtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu na wananchi wa Handeni  kufaidika navyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi.Fatuma Kalovya amesema Asasi hiyo ilianza kufanya kazi Handeni tangu mwezi septemba katika Kata nne ikiwepo Sindeni, Kwamatuku, Kwankonje na Kwaluguru na imewasidia sana vijana kwa kike kujielewa na kuwajengea ujasiri wa kujieleza bila woga.

Pia amewashukuru kwa kuchagua Wilaya ya Handeni na amewasihi kuendelea kutoa mchango wao kwa jamii ya Handeni na amesema vituo vya Afya hasa vilivyoko barabara kuu ikiwepo Mkata na Kabuku vimekuwa na mahitaji makubwa kwani wagonjwa ni wengi kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu pamoja na ajali za mara kwa mara

Kiongozi wa Asasi ya HOPE FOR YOUNG GIRLS Bi Salama Kikundo amesema tangu wameanza kufanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mwezi septemba walifanikiwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kike katika shule saba  ikiwepo shule za Sekondari tatu na Msingi nne na wamefurahi sana sehemu zote walizopita walipewa ushirikiano.

Akitoa takwimu ya vitu walivyotoa Bi Salama amesema wanatoa taulo za kike boksi 50, mashuka 200, mzani wa kupimia mtoto baada ya kuzaliwa 1, mashine za kupimia presha 3,mashine za kupima Kisukari 3, mipira ya vitanda vya kuzalia kina mama boksi 2, vifaa vya kumsaidia mama kujifungua 2 na kanga doti 50 ambazo zinathamani ya zaidi ya milioni 4.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dr. Ipyana Mwiluko ameishukuru Taasisi hiyo  kwa msaada wao kwa kuwa wamesaidia kupunguza changamoto kubwa hasa vifaa vya kina mama wakati wa kujifungua na watoto wachanga. Aidha amesema vituo vya Afya vya Kabuku na Mkata vinatibu wagonjwa zaidi ya mia moja kwa siku.

MWISHO.

Imeandaliwa na;

Paulina John

Kitengo cha Habari na mawasiliano Handeni DC

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bi.Upendo Magashi wa tatu kulia akipokea vifaa kutoka kwa kiongozi wa asasi hiyo Bi Salama Kikungo

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi.Fatuma Kalovya  wa kulia akipokea vifaa kutoka mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. Ipyana Mwiluko wa pili kulia akibeba moja ya vifaa alivyokabidhiwa na kuahidi kuvitunza

Picha ya pamoja baada ya kupokea vifaa

Afisa maendeleo ya jamii Bi.Rachel Mbelwa akitoa shukrani kwa shirika kwa kuja Handeni na kutoa vifaa hivyo 

Baada ya kukabidhi vifaa wlitembelea wodi ya wazazi na kuwagawia kanga





Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HANDENI DC June 04, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa