JUKUMU LA IDARA YA AFYA NI KUTOA HUDUMA KWA JAMII, HUDUMA AMBAZO ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI YAFUATAYO
• Afya Kinga; kukinga jamii dhidi ya magonjwa
• Tiba: kutoa huduma za tiba kwa magonjwa
• Ukuzaji wa Afya/Elimu ya Afya: Kuijengea jamii uelewa na kuishi maisha yanayopunguza uwezekano wa kupata maradhi mbalimbali.
• Rehabilitation: Kuwezesha mtu mwenye ulemavu wa kimaumbile/akili uliosababishwa na magonjwa/ugonjwa aweze kuishi maisha sawa au karibu sawa na wenzake.
• Lishe: Inalenga kukuza uelewa na kuishi maisha ambayo yanazingatia kanuni za lishe bora.
• Ustawi wa jamii: Kuwezesha jamii kupata haki sawa za kuishi katika Nyanja muhimu au haki za msingi za kibinadamu.
Idara inahakikisha huduma zinapatikana kwa kufanya yafuatayo kama idara katika Halmashauri ya Wilaya;
1. Kumshauri Mkurugenzi kwa masuala yote ya Afya katika Wilaya /Halmashauri
2. Kusimamia masuala yote ya kitalaamu ya afya kuanzia ngazi ya Wilaya/ Halmashauri mpaka kwenye jamii/ngazi ya kaya.
3. Usimamizi wa huduma za afya ndani ya Wilaya/ Halmashauri
4. Kusimamia na kuhakikisha huduma bora za afya na matibabu zinatolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri kuanzia ngazi ya Zahanati, vituo vya afya hadi Hospitali
5. Kuandaa taarifa zote za Afya za Wilaya/Halmashauri
6. Kusimamia Rasilimali zote za afya , yaani watushi, fedha, vifaa, majengo na dawa katika Halmashauri ngazi zote.
7. Kusimamia na kushauri katika kuandaa na utekelezaji wa mipango ya Afya ya Halmashauri kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya/Halmashauri, Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na wadau mbalimbali
AFYA KINGA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Majukumu hayo ni pamoja na:
Ukaguzi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara kama vile nyumba za kulala wageni,majengo ya kutengeneza na kuuza vyakula ili kuondoa machukizo yanayoweza kuhatarisha afya ya binadamu.
1. Utoaji wa elimu ya afya kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
2. Utoaji wa chanjo kwa magonjwa ya kuambukiza kwa wajawazito na watoto
3. Usimamizi wa afya na usalama mahala pa kazi
4. Usimamizi wa usafi wa Mazingira.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa