IDARA YA ARDHI NA MALIASILI.
Idara ya ardhi inamajukumu na huduma zifuatazo inazotoa kwenye Halmashauriya Wilaya ya Handeni.
MAJUKUMU YA IDARA YA ARDHI
1. Kusimamia sera,miongozo,sheria.taratibu na kanuni za uendelezaji naumiliki wa ardhi.
2. kusimamia sera, miongozo,sheria,taratibu na kanuni za uendelezaji wasekta ya misitu na hifadhi ya wanyamapori.
HUDUMA ZA KITENGO CHA ARDHI.
1. Kusaidia Vijiji kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi.
2. Kutoa hati miliki za viwanja, mashamba na maeneo ya uwekezaji.
3. Kufanya uthamini wa ardhi.
4. Kuandaa ramani na michoro ya mipango miji.
5. Kusimamia programu za uendelezaji za miji.
6. Kusaidia kutatua migogoro ya mipaka ya ardhi.
MAJUKUMU NA HUDUMA ZA SEKTA YA MISITU.
1. Kusimamia na kuendeleza misitu ya asili inayosimamiwa kisheria.
2. Kusimamia shughuli za usafishaji wa mashamba.
3. Kuto vibali mbalimbali vya uvunaji wa mazao ya misitu.
4. Kusimamia shughuli za upandaji miti.
MAJUKUMU NA HUDUMA YA SEKTA YA NYUKI.
A. Kuhamasisha jamii kuanzisha hifadhi za ufugaji nyuki.
B. Kutoa mafunzo ya uendelezaji wa Sekta ya ufugaji nyuki.
C. Kusaidia vikundi na watu binafsi kuongeza thamani ya mazao ya nyuki.
D. Kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa