IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI:
Idara ya Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili (2) ambazo ni:-
(i) Mifugo
(ii) Uvuvi.
MAJUKUMU YA IDARA:
Jukumu la Idara hii ni kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Serikali kuu na Wadau kutoka Sekta binafsi. Shughuli zinazofanywa na Idara ni pamoja na:-
1. Mifugo
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya mifugo na ufugaji kupitia huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya wafugaji.
Kusimamia na kuratibu huduma za kinga na tiba kwa mifugo zitolewazo na Halmashauri, Serikali Kuu na sekta binafsi.
Kusimamia ukaguzi wa nyama na mazao yatokanayo na Mifugo usimamizi wa usafi wa mazingira ya machinjio zetu ndogo za mifugo.
Kusimamia utoaji wa vibali mbali mbali vya kusafirishia mifugo na Mazao ya Mifugo ndani ya nchi.
Kusimamia vituo vya kukusanyia maziwa
. Kuunda na kusimamia sheria ndogo ya kuingiza na kutoa mifugo Wilayani
. Kufanya utambuzi, ufuatiliaji na usajili wa mifugo
. Kutenga na kuendeleza maeneo ya nyanda za malisho
. Kuwezesha Mpango wa matumizi bora ya Ardhi vijijini.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa