WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZA DKT. SAMIA.
Watumishi Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wameungana kwapamoja kumpongeza na kutoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi na kuimarisha uchumi wa Tanzania hususani kwa Wilaya ya Handeni.
Tuzo hiyo ya kutambua mchango wa Rais Mhe. Dkt Samia imepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Mhe. Dkt. Batilda Burian kwa niaba yake na kuwapongeza wanawake hao kwa kuwa na uthubutu wa kufanya jambo hilo la kutambua mchango wa Rais katika kuleta maendeleo nchini.
Pia Balozi Dkt. Batilda amewataka wanawake hao pamoja na watendaji kuongeza kasi ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yao ili hii tuzo iweze kuwa na thamani zaidi niwaombe muongeze kasi zaidi ya kutatua kero zinazowakabili wananchi lakini pia muendelee kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha wanawake hao wametoa tuzo kwa Katibu tawala Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema pamoja na tuzo kwa Katibu tawala Wilaya ya Handeni Bi. Magerth Killo kwa kutambua michango yao kama wanawake katika kusimamia utekelezaji wa Maendeleo na kukabidhiwa pikipiki tatu kwa watumishi wanawake ambao Maafisa watendaji wa Kata za Mazingara, Mkata na Kabuku kwa lengo la kuwarahisishia utendaji wao wa kazi zao.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando amesema katika Wilaya ya Handeni ameendelea kupokea pesa kutoka Serikalini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu, Afya, Maji na Barabara na Serikali ya Mhe Rais Dk Samia imefanya mambo makubwa katika uboreshaji wa huduma za kijamii, na kutekeleza ahadi zilizotolewa kuhusu miradi ya maendeleo. Msando Alisema.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa