IDARA YA MAJI
Idara ya maji imegawanyika katika sehemu kuu tatu zinozoongozwa na Wahandisi wa maji na ujenzi kama ifuatavyo;
1. Mipango na usanfu,
2. Ujenzi,
3. Uendeshaji na matengenezo.
MAJUKUMU YA SEHEMU ZA IDARA YA MAJI NI KAMA IFUATAVYO:-
1. Mipango na usanifu
Sehemu ya mipango na usanifu inahusika na:
i. Kupanga na kuratibu mzunguko wa maendeleo ya miradi ya maji (project circles) kwa wananchi katika sekta za umma na watu binafsi kuhusu usambazaji maji wilayani.
ii. Kuainisha mpango wa maendeleo ya miradi ya maji na bajeti ya mwaka ya Halmashauri ya wilaya na mpango wa maendeleo ya sekta ya maji wa Taifa.
iii. Kumshauri Mhandisi wa maji wa Wilaya kuhusu kupata Mhandisi mshauri wa kufanya upimaji na usanifu wa miradi ya maji anapohitajika.
iv. Kutathmini miradi ya maji vijijini kutokana na maombi ya vijiji.
v. Kutoa utaalam kuhusu upimaji na usanifu wa miradi ya maji kwa wadau wanaohusika na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani.
vi. Kuainisha usanifu wa ujenzi wa miradi na usanifu wa teknolojia ya uendeshaji na matengenezo ya miradi wakati wa utayarishaji wa mipango ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi.
vii. Kufuatilia na kuhakiki usanifu unaofanywa na waandisi washauri binafsi walioingia mkataba na Halmashauri au vijiji kwa kazi husika.
viii. Kushauri vijiji kuhusu jinsi ya kushiriki kikamilifu katika kuchagua na kutayarisha miradi ya maji.
ix. Kusaidia utayarishaji wa mapatano na makubaliano baina ya wilaya na vijiji, au vijiji na wakandarasi, kwenye kutekeleza miradi ya maji mahali ambapo wakandarasi wanatumika.
x. Kuratibu na kutoa ushauri unaohitajika kwenye jumuiya ya vijiji kwenye utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji.
xi. Kukusanya takwimu mbalimbali kutoka vijijini na kuzifanyia kazi ili zifikie hatua ya kuwa taarifa zinazoweza kafanyiwa kazi.
xii. Kuweka takwimu zote za miradi ya maji za Halmashauri na sekta binafsi ili kusaidia katika kupanga miradi mbalimbali wilayani.
xiii. Kuhamasisha maendeleo ya wananchi kwa kuhifadhi na kutumia rasilimali ya maji.
xiv. Kuhifadhi taarifa kwenye kompyuta na kuzisambaza taarifa hizo zonakohitajika (ndani na nje ya ofisi ya mhandisi wa maji wa wilaya).
xv. Kufanyia uchambuzi na kutathmini mfumo wa utunzaji habari na kuboresha mfumo wa kutunza kumbukumbu hizo.
xvi. Kuandaa taarifa za kila mwezi kuhusu shughuli za sehemu ndogo.
2. Ujenzi
Sehemu ya ujenzi ina majukumu yafuatayo:
i. Kutayarisha, kuratibu na kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji inayojengwa na Halmashauri ya wilaya kwa kushirikisha wananchi.
ii. Kutayarisha taratibu na miongozo mbalimbali ya ujenzi wa miradi ya maji itakayojengwa na wakandarasi au sekta binafsi
iii. Kusaidia vijiji kutayarisha mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa kushirikisha sekta binafsi.
iv. Kusaidia timu ya wilaya inayoshughurika na masuala ya maji na usafi wa mazingira kutayarisha zabuni mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maji ikiwa ni pamoja na ile ya sekta binafsi.
v. Kufuatilia na kusimamia wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya maji walioajiriwa na Halmashauri ya Wilaya.
vi. Kuratibu na kutayarisha miongozo mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa ajili ya vijiji.
vii. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi kuhusu ujenzi wa miradi ya maji inayojengwa na wakandarasi.
viii. Kuandaa taarifa kuhusu kazi za ujenzi wa miradi yote ya maji wilayani ya Halmashuri na sekta binafsi.
ix. Kuratibu na kusimamia utunzaji wa mazingira wa vyanzo vya maji.
x. Kukagua na kutathmini hali ya mazingira kabla na baada ya mradi kujengwa ili kuepusha uchafuzi na uharibifu wa mazingira.
xi. Kuchukua hatua zinazostahili baada ya ukaguzi kufanyika kwa lengola kuepusha na kurekebisha endapo uharibifu umejitokeza.
xii. Kushiriki katika kutoa elimu ya afya na usafi wa mazingira kwa jamii wakati wa ujenzi wa miradi ya maji.
xiii. Kuelimisha jamii kuhusu uondoshaji wa maji yaliyotumika, matumizi bora ya maji na ujenzi wa vyoo bora.
xiv. Kukagua, kushauri na kusaidia jamii katika utunzaji wa mazingira.
xv. Kuhakikisha usafi wa mazingira katika vyanzo vya maji ili kulinda afya za watumiaji wa maji.
3. Uendeshaji na Matengenezo.
Sehemu ya Uendeshaji na Matengenezo ina majukumu yafuatayo:
i. Kusanifu namna za kufanya matengenezo, taratibu na mbinu.
ii. kutekeleza utaratibu uliopangwa kufanyika matengenezo ya kazi na kukabiliana na matatizo ya Vifaa.
iii. Kubaini matatizo yanayojitokeza katika miradi ya maji na kuyatafutia ufumbuzi.
iv. Kubadilisha baadhi ya vifaa na kuhakikisha mradi unafanya kazi kwa.
v. Kufanya ukaguzi wa miradi ya maji inayotoa huduma.
vi. Kuhakiki vifaa vya matengenezo.
vii. kufuatilia na kudhibiti gharama za matengenezo katika miradi ya maji.
viii. kukabiliana na matatizo ya dharura, na kufanya matengenezo.
ix. Kuandaa mipango ya matengenezo kwa miradi inayohitaji kufanyiwa ukarabati.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa