HANDENI DC IMEFANYA BARAZA LA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024.
Baraza hilo la madiwani limefanya kikao chake kilichoongizwa na Mwenyekiti Mhe. Mussa Mwanyumbu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Katika baraza hilo waheshimiwa madiwani walisoma taarifa za Kata kwa sekta za elimu, afya, kimo, mifugo, michezo na utawala bora zikionesha mafanikio, changamoto na utatuzi wa changamoto hizo.
Pia sekta ya barabara (TARURA), maji (RUWASA) na TANESCO walitoa taarifa za utekelezaji wa shughuli zao na wajumbe wakaomba hizo sekta kufanya upembuzi yakinifu wa maeneo mbalimbali ili kutatua kero za barabara, maji na umme kwa kuwa maeneo mengi yana changamoto ya huduma hizo.
Wakati wa mawasilisho ya taarifa zao, madiwani wameushukuru Mpango wa TASAF kwa kuwasaidia wananchi kupitia miradi ya ajira za muda kwa kujenga miundombinu ya maji na barabara vijijini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu, kushoto wa kwanza.
Ndg. Saitoti Z. Stephen, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa