KITENGO CHA SHERIA
UTANGULIZI.
Kitengo cha sheria ni miongoni mwa vitengo vinavyounda Idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Majukumu ya Kitengo cha Sheria ni kama yafuatayo:
1. Kutoa ushauri kwa Halmashauri ili kufikia maamuzi mazuri ambayo humaliza migogoro.
2. Kutunga sheria ndogo za Halmashauri
3. Kuandaa miswada ya sheria ndogo za vijiji kulingana na mahitaji ya Halmashauri au kufuatana na maelekezo tunayopokea.
4. Kuhudhuria kesi mbalimbali Mahakamani zinazoihusu Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri za vijiji na kutoa utetezi kwa mujibu wa sheria (Legal Advocacy Defence)
5. Kutoa taarifa mbali mbali za migogoro ya kisheria inayoihusu Halmashauri.
6. Kusaidia Kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi vijijini baina ya wao wenyewe au serikali za vijiji kwa mujibu wa sheria za Nchi.
7. Kuhimiza na kusimamia utawala wa sheria ndani ya Halmashauri na katika serikali za vijiji ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na migogoro kumalizika.
8. Kufuatilia misuada, waraka au marekebisho ya sheria zinazohusu maslahi ya Halmashauri na kutoa taarifa kwenye Halmashauri kwa wakati.
9. Kufanya upekuzi wa mikataba mblimbali ya manunuzi katika Halmashauri.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa