MAJUKUMU YA IDARA ZA KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA.
1. Kuboresha Huduma za ugani kwa wakulima katika vijiji 91 vya Halmashauri ya Wilaya.
2. Kujenga na kuiendeleza miundombinu ya umwagiliajji
3. Kuendeleza matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea, Matumizi ya mbegu bora na viuatilifu.
4. Kuendeleza matumizi ya zana bora za kilimo kwa kusaidia uwezeshaji wa matrekta makubwa na kuayasambaza kwa wakulima vijijini.
5. Kuanzisha mashamba darasa katika vijiji vyote ili kueneza mbinu za bora za kilimo
6. Kuendeleza teknolojia za usindikaji na hifadhi ya mazao ili kuongeza thamani na kuboresha mfumo wa masoko .
7. Kuendeleza kilimo cha mazao ya biashara (Machungwa,Maembe na Katani)
8. Kuwawezesha Wakulima kushiriki maonesho ya nanenane ya kanda ya Mashariki.
9. Kuwezesha mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini.
10. Kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika wa wakulima AMCOS na SACCOS.
11. Kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama na wasio wanachama wa vyama vya ushirika.
12. Kuviunganisha vyama vya ushirika na wadau wengine( TAASISI ZA FEDHA Kuboresha afya ya Mifugo kwa kutoa kinga dhidi ya maradhi mbali mbali.
HUDUMA ZINAVYOPATIKANA
Huduma hizi hutolewa Halmashauri ya Wilya ya Handeni kama ifuatavyo.
• Kupata ushauri wa moja kwa moja toka ofisi ya Kilimo, Umwagiliaji na ushirika katika Wilaya.
• Kupata ushauri wa ana kwa ana toka kwa wataalam wa wilayani, Kata au kwenye Vijiji katika shamba la mkulima
• Kupata ushauri toka ofisi ya kata au ya Vijiji.
• Mafunzo kwa njia ya mikutano ( warsha na semina mbalimbali)
• Mafunzo kwa njia ya vikundi kuongea na vikundi
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa