Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mussa Mwanyumbu limefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa lengo la kujifunza na kuongeza uwezo wa kuisimamia Halmashauri katika maswala ya Kiutawala , Uzalishaji wa Hewa ya ukaa, kubuni vyanzo vipya vya mapato. kujifunza namna ya kuiendasha na sasa wanaenda kuhakikisha Halmashauri inakuwa kinara katika nyanja zote za ukuaji kiuchumi.
Baada ya kutembelea na kuona Miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Tanganyika Mhe. Mwanyumbu amesema kutokana Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato, mapato yatokanayo na mauzo ya Hewa ukaa hivyo chaguo lao limegusa mahitaji na wanenda kuyatumia yote waliyoyapata na kuboresha Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando ambaye pia alikuwa ni Miongoni mwa waliofanya ziara hiyo amewataka Madiwani na Wataalam kutumia elimu ya mafunzo waliyoipata ili iweze kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Katika ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe. John Sallu aliyekuwa miongoni mwa ziara hiyo amesema ziara hiyo imelenga kuwapatia mafunzo Madiwani kwa lengo la kuona wenzao namna wanavyozisimamia Halmashauri pamoja na namna ya kukusanya mapato.
Akizungumza wakati wa mapokezi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Alex Mrema ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema kuwa tumeguswa na ziara yenu kwasababu ziara hiyo itasaidia kuboresha utendaji wa kazi baina ya Halmashauri yatu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni “ Aliwakaribisha”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Stephen amesema kwamba tumefanikiwa kufanya ziara katika Halmashauri ya Tanganyika na kujifunza namna wanavyokusanya mapato yatokanayo na mauzo ya hewa ukaa, kuona mbinu za ukusanyaji Mapato ya Halmashauri, kuona jinsi vijiji vinavyonufaika na Mapato ya hewa ukaa ikiwa ni pamoja na wananchi zaidi ya 34,000 wamilipiwa bima ya afya katika vijiji 8.
.
Aidha Bw. Saitoti alisema ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato hayo inahitaji ushirikishwaji, kuwawezesha wakusanyaji wa mapato ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo ili waweze kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa . “ Alibainisha.”
Kwa upande wa Madiwani walitoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kuandaa ziara ya mafunzo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali na namna ya usimaiaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwenye Halmashauri hizo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mussa Mwanyumbu, Kulia aliyevaa koti jeusi
Mhe. Albert Msando, Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Mhe. John Sallu, Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, wakwanza kushoto
Ndg. Saitoti Stephen (Wakwanza kulia) Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa