MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu Msingi kwa Halmashauri ikiwa ni pamoja na:
• Kuratibu ufundishaji na ujifunzaji katika shule zote za msingi za serikali na binafsi.
• Kuandaa taarifa zote za kielimu Idara ya Elimu msingi za ndani na nje ya Wilaya.
• Kuratibu shughuli zote za mitihani ya kawaida na kitaifa kwa shule za msingi za serikali na Binafsi.
• Kuratibu shughuli zote za Michezo ya shule za Msingi (UMITASHUMTA) ngazi ya shule hadi taifa.
• Kusimamia shughuli zote za Elimu ya Watu wazima katika Halmashauri
• Kusimamia shughuli zote za Elimu Maalum katika Halmashauri.
• Kuratibu shughuli za afya na lishe ya wanafunzi shuleni.
• Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule za serikali.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa