Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
Idara hii ni mojawapo ya Idara 13 zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni yenye majukumu yafuatayo:-
1. Kutoa ushauri wa kuandaa Mipango na miradi ya maendeleo kisekta katika idara zilizopo Halmashauri;
2. Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuunganisha takwimu za kijamii na kiuchumi katika Wilaya;
3. Kusaidia sekta mbalimbali katika shughuli za kuainisha, kutathmini na kuibua miradi ya maendeleo;
4. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mipango na kuhuisha mipango hiyo katika vipindi mbalimbali;
5. Kuhakiki na kuunganisha Mipango na Bajeti ya Halmashauri pamoja na Miradi ya maendeleo;
6. Kuandaa Mpango Mtiririko wa fedha wa Bajeti ili kuilekeza Serikali kuu katika kugawa fedha na kutekeleza miradi kwa wakati;
7. Kuandaa na kuunganisha taarifa za utekelezaji za miradi ya maendeleo na taarifa za kifedha za robo mwaka na mwaka mzima;
8. Kutoa ushauri kwa jamii juu ya masuala ya maendeleo kuhusiana na sera mbalimbali za kisekta kama Sera za Kilimo, Mifugo, Afya n.k
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa