• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025, MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI AWAFUNDA VYAMA VYA SIASA HANDENI

Imerushwa: September 15th, 2025

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imevitaka vyama vyote vya siasa katika Wilaya ya Handeni kuhakikisha vinazingatia kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, uwazi na kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kikao kazi na wawakilishi wa vyama vya siasa katika Wilaya ya Handeni, Bi. Edna Assey kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa alisema kuwa jukumu la vyama vya siasa ni kuhakikisha vinashiriki uchaguzi kwa kuzingatia misingi ya kidemokrasia na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha uhalali wa mchakato mzima.

"Vyama vya siasa haviruhusiwi kujihusisha na vitendo vya rushwa kama kutoa fedha, mikopo, zawadi au hata ahadi za vyeo kwa lengo la kushawishi wapiga kura. Kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kinaweza kupelekea hatua kali za kisheria kuchukuliwa,” alisema Bi. Edna

Aidha, aliwakumbusha viongozi wa vyama kuzingatia haki na wajibu wao wakati wa kampeni, ikiwemo kuendesha kampeni za kistaarabu, kuheshimiana na kuepuka kutumia lugha za matusi, kejeli, uchochezi au vitisho dhidi ya vyama vingine.

Ofisi ya Msajili imeeleza kuwa uchaguzi ni zoezi la kitaifa linalohusu mustakabali wa taifa lote, hivyo vyama vyote vinapaswa kushiriki kwa kuonyesha mfano bora wa uongozi unaojali maslahi mapana ya wananchi na taifa.

Bi. Edna Assey alisisitiza kuwa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa kutasaidia kujenga mshikamano wa kitaifa, kuimarisha demokrasia na kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pia imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa kutumia haki ya kupiga kura na kufanya maamuzi kwa uhuru bila kushawishiwa kwa rushwa au vitisho. Wananchi wamehimizwa kutanguliza amani na mshikamano na wa kitaifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.


Bi. Edna Assey(kushoto) kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini akitoa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Handeni


Viongozi wa vyama vya Siasa Wilaya ya Handeni






Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025, MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI AWAFUNDA VYAMA VYA SIASA HANDENI

    September 15, 2025
  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa