Sekta ya Mifugo
Halmashauri imeanza mikakati mahususi ya kuendeleza sekta ya mifugo kwa kuwahusisha wafugaji wahamaji katika ufugaji wa kisasa unaozingatia ubora wa mifugo na malisho. Idadi ya mifugo katika sensa iliyofanyika mwaka 2014 ni kama ifuatavyo: wapo ng’ombe 125,780, mbuzi 189,141, kondoo 38,166, kuku 378,565, nguruwe 1,155, punda 1,372 na mbwa 8,124.
Lengo la uboreshaji wa mifugo ni kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2021 wananchi wawe na uwezo wa kuuza mifugo na nyama nje ya nchi, hii itabadilisha hali ya maisha kwa wafugaji na kuondokana na ufugaji wa kuhama hama.
Aidha, katika uboreshaji wa mifugo, yapo madume bora ya ngombe 1,800, mabeberu ya kisasa 920 na majogoo ya kisasa 2,400 ambayo yanatumika kwa ajili ya uboreshaji wa mifugo. Uhamilishaji ni njia nyingine inayotumika kuboresha ng’ombe, ambapo Halmashauri imejiwekea malengo ya kuhamilisha ng’ombe 2,000 kwa mwaka. Kwa mwaka 2015/2016 ng’ombe 174 wamehamilishwa.
Halmashauri ina vitalu vyenye ukubwa kati ya hekta 3,000 hadi 4,000 kila kimoja, pia imetenga maeneo kwa ajili ya kuanzisha ranchi za kijamii (community ranches) kwa ajili ya wafugaji wadogo. Kwa maana hiyo, tumewahimiza wamiliki wa vitalu kuweka sehemu ya kunenepeshea mifugo (feedlot ting) ili waweze kunenepesha mifugo ya wafugaji wa kawaida kwa maelewano maalum. Jedwali lifuatalo hapo chini linaonesha aina ya ranchi au vitalu vya wafugaji vilivyopo hapa wilayani.
Aina ya ranchi/kitalu |
Aina ya mifugo |
||
Ng’ombe |
Mbuzi |
Kondoo |
|
Mzeri Hill Ranchi (NARCO)
|
2,500 |
60 |
200 |
Nkale Ranchi
|
306 |
513 |
0 |
Olosipa farm
|
1,300 |
180 |
150 |
Sado farm
|
50 |
250 |
250 |
Major One farm
|
200 |
0 |
150 |
Shalom farm
|
400 |
0 |
0 |
Good chance farm
|
400 |
0 |
0 |
Mukuti farm
|
1,000 |
0 |
0 |
Stage farm
|
400 |
160 |
0 |
Klub Africo farm
|
120 |
0 |
0 |
Jumla |
6,676 |
1,163 |
750 |
Eneo la malisho ni hekta 367,530 ambazo zina uwezo wa kulisha takriban ng’ombe 200,000. Hata hivyo eneo hilo linatumika kwa shughuli mbalimbali za kilimo, makazi na migodi hivyo kusababisha migogoro kati ya wafugaji na wadau wengine wanaotumia ardhi. Jitihada zinazoendelea ni kuainisha upya maeneo ya malisho kupitia mipango ya matumizi bora ya ardhi na hadi sasa Vijji 21 vimetengenezewa na kuainisha maeneo ya malisho katika mpango wa matumizi bora ya ardí, Lengo hadi 2025 likamilike vijiji vyote.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inamifugo ya aina mbalimbali ikiwemo;
1. Ngombe
2. Mbuzi
3. Kondoo
4. Nguruwe
5. Ufugaji wa kuku wa kienyeji.
6. Punda
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa