Taasisi ya kiraia ya (Strategis Insurance) ambayo makao makuu yake yako Dar es Salaam yafanya ziara ya siku mbili wiki iliyopita katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni zikiwepo shule za msingi, Mhalango, Tuliani kwachaga, Komkonga, Suwa, Mkomba na shule za Sekondari Mkata, Kitumbi na Kisaza pamoja na vituo vya afya ikiwepo zahanati ya Kwangahu kuona changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo.
Mkuu wa Wiliya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ameishukuru taasisi ya (Strategis Insurance) kwa kuichagua Handeni kufanya tathmini ya changamoto katika sekta ya elimu na afya na kuwapongeza kwa juhudi zao za kumuunga mkono Mh. Rais Dr John Pombe Magufuli kwenye juhudi zake za maendeleo nchini.
Wakati wa ziara hiyo katika shule ya sekondari Kisaza ambayo ndiyo imeanzisha kidato cha tano na sita, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ameahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano(500,000) kwaajili ya kuongezea vitabu vya kidato cha tano na kuwaahidi wanafunzi uangalizi wa karibu pale wanapopata changamoto ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Pia Mh. Godwin Gondwe amemuagiza afisa elimu sekondari kusimamia wanafunzi kutumia lugha ya kiingereza kama lugha ya mawasiliano shuleni ili kujibu mitihani yao kwa ufasaha kwakua masomo mengi yanatumia lugha ya kiingereza.
Pamoja na changamoto mbalimbali Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe amewapongeza walimu kwa kufanya juhudi kubwa kwenye suala zima la ufundishaji na kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 kwakuwa Halmashauri imeshika nafasi ya tatu kati ya Halmashauri 11 za kielimu zilizopo mkoni Tanga.
Mkuu wa kitengo cha masoko wa taasisi ya (Strategies Insurance) Bwana Denis Nombo amesema lengo la ziara yao ni kufanya tathmini ya changamoto zinazokumba sekta ya elimu na afya na kwamba wameona uhitaji mkubwa wa miundombinu wa Madarasa, matundu ya vyoo, maji, maabara, ofisi za walimu na madarasa ya elimu maalumu, hivyo amesema watalifanyia kazi ili waweze kupunguza changamoto hizo.
Naye Afisa masoko wa wa taasisi hiyo Dkt. Lilian Malakasuka amefurahishwa na namna wanafunzi wanavyopata chakula cha mchana shuleni na kuwapongeza Mh. Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kwa namna wanavyosimamia upatikanaji wa chakula shuleni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliishukuru taasisi hiyo kuja kufanya tathimini ya changamoto ya sekta ya elimu na afya katika Halmashauri yake.
Wakati timu hiyo ilipotembela shule ya sekondari Kisaz na wanafunzi wa kidato cha tano kutoa changamoto za uchache wa vitabu vya sanaa, aliahidi kurudufisha vitabu vya masomo hayo ili kupunguza upungufu wa uchache wa vitabu hivyo hapo shuleni.
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji amewahakikishia wanafunzi wa Kisaza kuwa kwenye ajira mpya ya mwaka huu Kisaza itapewa kipaumbele cha kupewa walimu wa sayansi kutokana na uhaba wa walimu wa kada hiyo kwa kidato cha tano na sita.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe alihitimisha kwa kusema kuwa hapo awali wananchi wa Handeni walikuwa hawawezi kujitolea ila baada ya kutoa elimu ya kutosha wananchi wameanza kujitolea kwenye ujenzi wa miundo mbinu na utoaji wa chakula shuleni.
Afisa elimu sekondari Bw. Gosbert Damazo na afisa elimu msingi Bw. Goodluck Mwampashi wameiomba taasisi ya (Strategis Insurance) iwasaidie kutatua changamoto kama ambavyo wameona kwenye ziara yao ya kufanya tathmini hiyo sekta ya elimu ufaulu uongezeke kutokana na miundombinu rafiki ya ujifunzaji kwa wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa wilaya Handeni Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mhalango.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe pamoja wataalam na wawakilishi wa Halmashauri ya Handeni wakikagua jengo la bweni la shule ya sekondari Kisaza.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akiwatoa hofu wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Kisaza.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe akishiriki chakula cha mchana na wanafunzi wa sekondari ya Kitumbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe akiongea na wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Kisaza.
Timu ya kufanya tathimini wakikagua majengo ya madarasa ya shule ya msingi Mkomba.
Afisa masoko wa taasisi ya Strategis Insurance Dr. Lilian Malakasuka akizungumza katika zira hiyo.
Mkuu wa kitengo cha masoko wa Strategis Insurance Bw. Denis Nombo akizungumza.
Timu ya kufanya tathimini wakikagua ujenzi wa choo cha shule ya msingi Suwa
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Gondwin Gondwe wa kwanza kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Halmashauri pamoja na viongozi wa taasisi ya (strategis Insurance).
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa