Baraza la kufunga mwaka Handeni kwa pamoja limeridhia makao mkuu ya Halmashauri ya Wilaya kujengwa Mkata.
Vikao vya Baraza la madiwani vya kufunga maridhiano hayo yamekuja baada Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe kuliekeza Baraza hilo maelekezo aliyoyatoa Naibu Waziri wa Tamisemi Mh. George Kakunda tarehe 17/08/2018 alipokuja katika ziara yake Mkoani Tanga kuhusu wapi hasa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kupitia mapendekezo ya ngazi mbalimbali ikiwepo Baraza la madiwani ikizingatia kanuni, taratibu na sheria
Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa baadhi ya vikao vimesahakaa kama Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Baraza kuu la Wilaya hivyo imebaki Baraza la Diwani.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe alisema kuwa ili Makao makuu ya Halmashauri yajengwe lazima izingatiwe suala la maelekezo ya Serikali, kuhalalisha vikao vinavyopaswa kukaa, uwepo wa taarifa ya kitaalamu iliyochanganua kwa kina, kutokuwepo na viashiria vya migogoro na maslahi mapana ya wananchi ikiwepo huduma za jamii pamoja na huduma za kiutawala.
Pia Mkurugenzi alitoa ufafanuzi kuwa vikao vya kisheria kujadili ni wapi pawe makao makuu ya Halmashauri havijawahi kukaa tokea mwaka 2012, vikao hivyo ni pamoja na timu ya kitaalamu vya kuchambua kwa kina mahali panapofaa kwa mujibu wa sheria, hivyo aliwataka madiwani kutumia nafasi waliyopata vizuri kuchagua mahali panapofaa kuwa makao makuu ya Halmashauri kwa kuzingatia maoni ya kitaalamu
Aidha utafiti ulifanyika katika miji midogo ambayo ni Mkata, Kabuku na Michungwani kwa lengo la kubaini eneo lipi hasa linafaa kujengwa Makao makuu ya Halmashauri kwa kuzingatia vigezo vinavyohitajika kama ukubwa wa maeneo au ardhi, uwepo wa huduma za kijamii, unafuu wa gharama wanayotumia wananchi kutoka maeneo mbalimbali kufika katika eneo la utawala, Idadi na msongamano wa watu na huduma za kiuchumi na kifedha.
Utafiti huo uliofanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 30/08/2018-07/10/2018 na kamati ikabaini kuwa mji mdogo wa Mkata unafaa kujengwa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kutokana na kuwa na ardhi ya kutosha ambapo una hekta 34513 na una msongamano mdogo wa watu ukilinganisha na ukubwa wa ardhi, zipo huduma za kifedha kama benki na SACCOS, huduma kijamii,pia unafikika kwa urahisi kwa wananchi wanatoka maeneo mbalimbali kwa gharama nafuu ukilinganisha na miji mingine
Wajumbe wa Baraza la Madiwani walipiga kura za wazi baada mwenyekiti wa kamati ya utafiti kusoma maoni ya kamati ya utafiti wa eneo la kujenga Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo wajumbe 25 kati ya 26 walichagua mji mdogo wa Mkata kujengwa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na mjumbe moja alipinga.
Kikao cha Baraza la kufunga mwaka kilifanyika kwa siku mbili tarehe 19-20/9/2018
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa