Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya limeridhia kufukuzwa kazi kwa watumishi wa Halmashauri 45 kwa makosa mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo kutoa taarifa za uongo kwa Mwajiri, Kukosa sifa za Kimuundo, utoro kazini na kughushi vyeti.
Akitoa maamuzi hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mustafa Beleko alisema, “ Watumishi walitoa taarifa za uongo 10 Halmashauri hii imewafukuza kazi, Waliojipatia ajira bila sifa za kimuundo ni 7 nao halikadhalika tumewafukuza kazi, na kuna watumishi 24 waliogushi vyeti nao halikadhalika tumewafukuza kazi, watumishi 4 waliofanya utoro kwa zaidi ya siku 5 mfululizo nao tumewafukuza kazi”.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Handeni Bi. Fatuma Kalovya alisema kuwa sekta zote zimeguswa na maamuzi ya Baraza kwa kufukuzwa kazi kwa Watumishi na hivyo kuwasisitiza watumishi waliobaki kuwa makini na kuzingatia weledi wa kazi wasije wakapatwa na janga hilo.
Baraza pia lilijadili mambo mbalimbali yanayohusu Halmashauri kama umeme, maji, Vitambulisho vya Taifa na barabara ambapo wataalam wa Sekta hizo walitolea ufafanuzi mambo yote yanayohusu sekta zao kwa maendeleo ya Halmashauri ya wilaya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa