Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nne imezinduliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe ambaye alikuwa mgeni rasmi, Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya wakati wa kutoa mafunzo kwa wadau na baadaye katika shule ya msingi Sindeni ambapo wasichana wenye umri wa miaka kumi na nne walipewa chanjo hiyo .
Lengo la chanjo hiyo ni kuwakinga wanawake na kensa ya kizazi mapema ambapo Tanzania ni nchi mojawapo Barani Afrika yenye idadi kubwa ya wanawake wenye saratani ya mlango wa kizazi na inakadiriwa na Shirika la Afya Duninani kuwa takribani wanawake elfu hamsini (50,000) wanapata saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amesema kuwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni kampeni ya kitaifa ili vijana wetu wa kike wawe na afya bora na kwamba hii chanjo watapatiwa mara mbili yaani kila baada ya miezi sita ili kukamilisha dozi na baada ya hapo hawataweza kupata kabisa saratani ya mlango wa kizazi “mpate hii chanjo,hii ndiyo kinga yenyewe ili muweze kuwa salama” alisema.
Pia wamewataka wazazi waliokuwepo kuwa mabalozi kwa watu wengine ili vijana wao wa kike wapate chanjo hiyo ya mlango wa kizazi na amesema kuwa tutaanza na wasichana wenye umri wa miaka kumi na nne waliokaribia kuvuka umri wa kupata chanjo hii na kwa kuwa chajo hii ni endelevu itatolewa kwa vijana wa kike wote wenye umri kuanzia miaka tisa hadi kumi na nne.
Amewaeleza pia wadau kuwa chanjo hii inatolewa bila malipo yoyote na wala haina madhara yoyote na kwamba tatiti kutoka Hospitali ya Ocean Road ambayo ndiyo pekee inafanya kazi kubwa ya kutibu saratani zinaonyesha kuwa 36% ya vifo vya wanawake vinasababishwa na saratani ya mlango wa kizazi na asilimia 50% ya vifo vya kina mama Tanzania husababishwa na saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti hivyo wawahimize wazazi waweze kuwapeleka vijana wao wa kike kupata chajo hii ya saratani ya mlango wa kizazi ili waepukane na ugongwa huo kwani ugonjwa mbaya sana.
Kwa upande wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dr. Credianus Mgimba wakati akitoa mafunzo kwa wadau amewaeleza kuwa Tanzania ina hali mbaya ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kuliko nchi zingine Barani Afrika na kwamba kwa mwaka wanawake 7523 husajiliwa wakiwa na saratani ya mlango wa kizazi pia asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi hujitokeza katika hatua ambayo tayari saratani imeshasambaa maeneo mengine ya mwili na kwamba wanawake wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI wanaathirika zaidi na saratani hii ya mlango wa kizazi.
Amesema lengo la Halmashauri ni kufikia asilimia zaidi ya 80 ya utoaji wa chanjo hii ya saratani ya mlango wa kizazi na itatolewa kwa uendelevu katika vituo vya afya vya serikali na binafs,mashirika ya dini, shuleni na kwenye jamii kwa hao vijana wa kike walegwa wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nne ambapo chanjo hiyo inafanyakazi kuliko waliozidi umri wa miaka kumi nne na watapata chanjo mara mbili kukamilisha dozi zitakazopishana kwa miezi sita.
Naye Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.Subira Makomaji ametoa mpango mkakati kuwa kwa mwaka huu wanatarajia kutoa chanjo hii kwa wasichana 3544 ambapo wasichana walioko shuleni watakuwa 2392 katika shule za msingi 142 kati ya shule 118 na shule za Sekondari zote 24 na wasisoma 1152 kupitia vituo vya afya na chanjo mkoba au tembezi na amewataka wadau kutoa ushirikiano ili kuwafikia walengwa wote.
MWISHO
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa