Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando ameunda kamati maalum ya uelimishaji, uhamasishaji na ushirikishaji wa jamii kuhusu kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Kamati hiyo inajumuisha wajumbe wafuatao; Mkuu wa wilaya ambae ndiye mwenyekiti,kamati ya ulizi na usalama, wataalam kutoka Halmashauri,viongozi wa dini,wanahabari,taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na wawakilishi wa wanajamii.
Mhe. Msando amesema kuwa kabla ya kuanza kazi kwa kamati hiyo amewataka wataalam waweze kuwajengea uwezo kamati na kuwapa maelekezo na mgawanyo wa majukumu ya kila mtu kwenye kamati kwa ajili ya kunusuru jamii ambayo ipo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko. Ameongeza kusema kwamba imezoeleka kuwa pindi inapotekea janga la mlipuko wa ugonjwa wanaachiwa viongozi lakini wapo watu ambao wanaushawishi na utaalamu wakiongea kwenye jamii inamuelewa na kufuata ushauri wake.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Albert Msando amewapongeza wajumbe hao na kuwaasa watumie uzoefu na ujuzi wao kuhakikisha jamii inakuwa salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen amepongeza zoezi zima la uundwaji wa kamati hiyo ambayo itaweza kusaidia kutoa elimu kwa jamii na amemwomba Mkuu wa Wilaya kuwa awaandikie barua wanakamati wote ili waweze kujijua, wajitambue na watambue majukumu yao ya kutoa elimu kwa jamii ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na homa ya matumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albart Msando
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Handeni.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Bi. Upendo Magashi Kulia akiwa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. Kanansia Shoo kushoto
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa