Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa CCM Halmashauri ya mji Handeni ambapo kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwepo Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Handeni,Wakurugenzi watendaji, Viongozi wa dini, Waheshimiwa madiwani, Wataalam wa Halamashauri ya Mji Handeni na Wilaya ya Handeni, Maafisa Tarafa, Watendaji Kata, Maafisa elimu Kata, wakuu wa shule na walimu wakuu.
Akizungumza katika kikao hicho Mh. Godwin Gondwe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema lengo la kikao hicho ni kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya lakini pia kuwakumbusha wadau hao namna ya kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mh. Gondwe amewataka viongozi wa Idara ya Afya kuhakikisha wanaandika dawa zote muhimu kwenye mbao za matangazo katika zahanati na vituo vya afya ili wagonjwa waweze kujua na amesema hii itasaidia wagonjwa wanaotumia kadi za bima ya matibabu iliyoboreshwa (ICHF) wasilalamike huku akiwataka Watendaji Kata kukagua kama orodha ya dawa hizo zimeandikwa.
Pia aliwataka Waganga wakuu kuhakikisha huduma ya kuandikisha wananchama wapya wa bima ya matibabu iliyoboreshwa (ICHF) inafanyika bila kusimama hii ni baada ya wadau kulalamika kutokuwepo kwa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo na kwamba zile Kata ambazo bado hazijazindua kampeni ya bima ya matibabu iliyoboreshwa wanafanya ndani ya mwezi moja
Aidha Gondwe amewamesihi wadau kushirikiana kupiga vita mimba na ndoa za utotoni ili watoto hao wa kike kufikia ndoto zao na amesema takwimu za mimba zipelekwe kila mwezi pamoja na kesi zote ambazo ziko ngazi ya Kata na vijiji wahakikishe wamepeleka ngazi ya Wilaya hii ni baada ya viongozi wa Idara ya elimu kusoma taarifa na kuonyesha kesi nyingi kuwa ngazi za vijiji na Kata kwa mda mrefu.
Alihitimisha kwa kuwataka Wakuu wa shule kuhakikisha wanafunzi wanaongea kiingereza hii baada ya kutembelea baadhi ya shule na kukuta wanafunzi hawajui kuongea lugha hiyo hivyo amewaekelekeza Wakuu hao wa shule wanafunzi kutokuongea lugha zingine wakiwa shule na kufanyika kwa midahalo mbalimbali kwa lugha ya kiingereza ili wanafunzi wajifunze kuongea lugha hiyo na kwamba hiyo itasaidia ufaulu kuongezeka.
MWISHO
Imeandaliwa na;
Paulina John
Kitengo cha Habari na mawasiliano Handeni DC
Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wadau elimu na Afya
Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Mwl. Boniphace Maiga akitoa neno la nasaha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akizungumza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Handeni akizungumza
Wataalam wa Idara ya afya Halmashauri ya Wilaya na Mji Handeni wakisoma taarifa za shughuli walizotekeleza
Watalaamu wa Idara ya Elimu Halmashauri ya Wilaya na Mji Handeni wakisoma taarifa za maendeleo ya elimu
Viongozi wa dini wakitoa ushauri ili Wilaya ya Handeni ifikie malengo yake
Wadau wakifuatilia mazungumzo ya kikao
Wadau mbalimbali wakiuliza maswali na kutoa ushauri
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa