Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe aliyasema hayo jana wakati wa kufunga zoezi la kutatua kesho za wananchi (ONE STOP JAWABU) katika viwanja vya shule ya msingi Kabuku ndani, kero hizo zilianza kutatuliwa kuanzia tarehe 16-18/12/2019 katika Kata ya Mkata na tarehe 19-21/12/2019 katika Kata ya Kabuku Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Mkuu huyo wa Wilaya Handeni alisema hivyo kwasababu idadi ya watu waliobaki wanaohitaji vitambulisho vya Taifa ni kubwa na wengi wao wametoka maeneo ambayo ni mbali na ofisi za NIDA hivyo kuwataka viongozi hao kutengeneza ratiba ya kuwafikia wananchi katika Kata zao na alisema ratiba hiyo ibandikwe katika ofisi za Kata, amesema ni haki ya kila mtanzania kupata kitambulisho cha Taifa.
Akitoa takwimu ya waliotatuliwa kero zao Mh. Gondwe amesema kwa siku tatu kwa Kata ya kabuku ambayo imejumuisha wananchi kutoka Kata za Komkonga, Kwedizinga, Gendagenda, Kabuku, Kabuku Nje na Ndolwa wananchi waliohudumiwa ni zaidi ya elfu tisini na sita(96000).
Alihitimisha kwa kuwataka viongozi wa idara ya Uhamiaji kushirikiana na viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili kuepusha usumbufu kwa wananchi na kupata huduma kwa wakati.
Kiongozi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Tanga Bw.Lembira Kitashu amesema baada ya zoezi la Kabuku wataanza na Kata za Kabuku, Kabuku ndani, Kwedizinga, Kitumbi, Segera, Mzundu na Komkonga hivyo aliwataka wananchi kurudi katika maeneo yao kwa kuwa watawafikia katika Kata zao.
Katika zoezi la utatuzi wa kero za wananchi (ONE STOP JAWABU) walikuwepo wataalamu mbalimbali wakiwepo viongozi wa vizazi na vifo (RITA), Idara ya uhamiaji, wataalamu mbalimbali kutoka Idara za Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na makampuni mbalimbali za simu.
MWISHO.
Imeandaliwa na;
Paulina John
Kitengo cha habari na mawasiliano Handeni DC
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wakati wa kufunga zoezi la kutoa majawabu kwa wananchi
kiongozi wa NIDA Mkoa wa Tanga Bw. Lembira Kitashu akiwatoa hofu wananchi.
Wataalamu mbalimbali wakitoa huduma kwa wananchi
Wananchi waliojitokeza kupata majawabu ya kero zao
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa