• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC HANDENI ATOA SIKU 14 KWA WATAALAMU WA ARDHI WA WILAYA KUAINISHA MPAKA BAINA YA HALMASHAURI YA MJI NA WILAYA KATA YA MISIMA

Imerushwa: November 20th, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amewapa siku 14 wataalamu wa ardhi wa Wilaya  kuainisha mipaka baina ya Kata ya Misima iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Halmashauri ya Mji ili kuondoa mkanganyiko wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu.

 Mkuu wa  Wilaya ameyazungumza hayo jana  alipokuwa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Msomera Kata ya Misima baada ya uongozi wa Kijiji hicho kuomba msaada wa kusikilizwa ili kuainishiwa mipaka baina ya Kata na Vijiji ili kuondoa muingiliano.


 Mh. Gondwe alisema kuwa wataalamuwa ardhi watapima na kuonesha mipaka baina ya Halmashauri ya Mji na Wilaya ili wafahamu mipaka yao na kutambua wanapaswa kuitika wapi na kuondoa migongano inayokwamisha wananchi kushiriki katika maendeleo.

 Alisema kuwa Msomera ni Kijiji kilichoanzishwa kisheria na kipo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hivyo wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa  kwa mujibu wa sheria na kuwataka wananchi wote wanaokuja kwenye Kijiji hicho na maeneo mengine kufuata masharti ya maeneo husika kwani Tanazania ni huru kuishi kwa kila mwananchi isipokuwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

 Aliongeza kuwa Kijiji cha Msomera kilitengwa maalumu kwa mifugo, wakulima ambao walikuwepo   kabla ya kijiji hicho kupangwa kuwa kwaaajili ya mifugo watambuliwe  na hawataondolewa, wakulima waliokuja baada ya kijiji kutambulika kuwa ni cha mifugo wataondolewa.

 Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka  wanakijiji cha Msomera kufuata utaratibu linapokuja suala la kuuza ardhi na kuingiza mifugo mipya kwa kushirikisha uongozi wa Kijiji na kufanya mikutano mikuu ya maamuzi ili kuwe na maaamuzi ya pamoja  hata kama  ardhi inayouzwa ni ya mtu binafsi. 

 “Kijiji kikipangiwa matumizi bora kitumike kama ilivyokusudiwa ili kuondoa migogoro, tunzeni ardhi yenu na rasilimali zenu  kwa ustawi wa vizazi vyenu,haijalishi kama mnaleta ndugu zenu, taratibu lazima zifutwe kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake” amesema Mkuu wa Wilaya.

Image may contain: 8 people, crowd, tree and outdoor

Baadhi ya Wakulima na Wafugaji walioshiriki mkutano huo.

Image may contain: 1 person, standing, tree, child, crowd and outdoor 

mmoja wa wafugaji akitoa malalamiko yake kuhusu wakulima kuvamia eneo la mifugo na kuanza kulima kinyume na taratibu na kuomba kuanishiwa mipaka kuepuka muingiliano.

Image may contain: one or more people, people sitting, crowd, tree, table and outdoor

Mkutano wa Hadhara ukiendelea  

Image may contain: 1 person, tree and outdoor

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe akiwaeleza wafugaji wa Kijiji cha Msomera kuwa  wakulima kuingia kwenye eneo la kufugia mifugo kunatokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waadilifu kwa kuuza maeneo bila kufuata taratibu na kuwataka kushirikisha wananchi kwa kila jambo kwani viongozi sio watu wenye maamuzi ya mwisho

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wafugaji  wa Kijiji cha Msomera na akiwasisitiza kuwa Kuwa Kijiji hicho ni cha wafugaji wote bila kujali kabila

Kaimu  Mkuu wa Idara ya  Ardhi na Maliasili Bw. Napoleone Mlowe akithibitisha kuwa Kijiji cha Msomera kinatambulika kisheria na ni eneo lililotengwa kwaajili ya wafugaji kulingana na mpango bora wa matumizi ya ardhi.

Diwani wa Kata ya Misima Mh. Mariamu Killo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msomera na kuwataka kuwa wavumilivu hadi hapo mipaka itakapoainishwa.
078: baadhi ya wafugaji na wakulima walioshiriki mkutano wa hadhara.





Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HANDENI DC June 04, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa