Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Stephen ameongoza watumishi kupanda Miti kwenye eneo la Makao Makuu ya Halmashauri, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na pembezoni mwa barabara inayoelekea kwenye majengo hayo.
Miche ya Miti ya aina tofauti tofauti Mia Mbili imepandwa hii leo kwenye maeneo hayo kwa lengo la kutunza mazingira kama kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 inasema “Tunza Mazingira, Okoa vyanyo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”
Bw. Saitoti amehimiza jamii kuyapenda Mazingira na kuyatunza na ametoa rai kutumia mvua hizi zinazoendelea kunyesha zitumike pia kwa kupanda Miti kwenye maeneo yao.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa