Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepokea miche 140000 kutoka Bodi ya Korosho na kugawiwa kwa wananchi bure kama zao biashara ili wananchi waondokane na umaskini kwani kwa miaka mingi zao kuu kwa Handeni lilikuwa mahindi.
Ambapo wananchi waliuza mahindi hayo kupata kipato cha kujikimu kitu kinachowasababishia kukosa chakula hivyo mwaka 2016/2017 viongozi wa Wilaya walitafuta mbinu mbadala ya wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kuchagua mazao mawili ya biashara ambayo ni zao Mhogo na Mikorosho na zao Mhogo lilifanikiwa kwa asilimia zaidi ya 70 kwani wananchi wamelima kwa wingi na kupata mafanikio.
Akizungumza katika uzinduzi wa upandaji wa Mikorosho ulioambatana na juma la upandaji miti uliyofanyika Katika Shule ya Sekondari Mazingara na baadaye katika Kijiji cha Mkata Mashariki jana , Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh.Martin Shigela ambaye aliwakilishwa na Mh.Godwin Gondwe Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema wameamua kuleta zao la korosho kama zao mbadala la biasahara kwa wananchi wa Handeni ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mgeni rasmi amewaeleza wananchi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mpaka sasa imepanda miche 20,000 ya mikorosho na leo imepokea miche 140000 na lengo letu nikufikia miche 300,000 ili wananchi waondokane na umaskini na pia kujipatia kipato cha muda mrefu na aliwaeleza wananchi malengo madhubuti ya kuanzisha zao hilo la Korosho kuwa ni kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwamba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo hatupaswi kulima mazao yanayostahimili ukame ili waondokane na adha ya kukosa chakula na kipato cha kukimu mahitaji yao.
Lengo lingine ni kuongeza na kuinua uchumi wa mwananchi moja moja kwamba mtu akiwa na shamba la korosho ataondokana na umaskini kabisa kwani atakuwa na maisha mazuri kwa kujenga nyumba nzuri,atasomesha watoto na atapata fedha za matibabu alisema” uzinduzi huu wa kilimo cha korosho maana ni kwamba umaskini kwaheri”
Pia amesema lengo lingine la kulima zao hilo ni kuongeza mali ghafi katika viwanda vyetu kwani anayezalisha mali ghafi ni mkulima na moja wa wakulima hao ni wakulima wa Handeni hivyo aliwaasa wananchi kusimamia matumizi na umiliki wa bora ya ardhi kwaajili ya uzalishaji wa mali ghafi hizo kwani baadhi yao wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na pia baadhi yao wamekuwa chanzo cha uuzaji wa ardhi kiholela hivyo wananchi wahahkikishe wanaunga mkono upandaji wa korosho kwa kasi ya Mh.Raisi. Aidha aliwashukuru askari JWTZ kutoka kitengo cha magari na usafirishaji makao makuu Dres-salaam kwa kuonyesha uzalendo wao kwenda kufuata miche hiyo ya mikorosh na pia kutoa malori yao bure kwaajili ya kubeba miche hiyo pia aliwapongeza viongozi wa Handeni na wananchi wote kwa kuunga mkono zoezi hilo la kuanzisha mazao ya biashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh.Ramadhani Diliwa amesema kuwa wananchi wa Handeni kwa miaka mingi wamekuwa wakilima zao moja la mahindi ambapo zao hilo halikutosheleza mahitaji yao na kuishi kwa mikopo ya kudumu kwani wakivuna wanalipa madeni na kuendelea kukopa hivyo aliwataka wananchi kutumia ardhi waliyojaliwa na mwenyezi Mungu kwani Handeni ina ardhi ya kutosha na kama sisi wakulima kipato chetu ni kilimo turudi kulima mazao ya uchumi kama Mihogo,Korosho,Michungwa,miembe mazao mabayo yanadumu zaidi ya miaka 50 aliesma”Tulimeni mazao ya biashara”.Amesema pia tunafanya hivyo ili Halmashauri ipate mapato ya ndani ya kutosha ambayo yatatumika kuwahudumia wananchi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe amewataka wananchi kuwa na utayari wa kilimo hicho cha korosho na kwamba hata kama miche hiyo itagawiwa bure lakini lazima anayepewa miche hiyo ataingia mkataba na Halmashauri kukiri kupokea na kuitunza kwa muda wote na endapo hataitunza miche hiyo atalipa fidia kwa kulipa shilingi 500 kwa kila mche hivyo kila mtu aelewe kuwa hatutoi miche hiyo kiholela lazima mtu awajibike kwa miche tuliyomkabidhi ili tuwe na uhakika wa miche kukua vizuri na kutunza na kwa upande Kata miche hiyo itakabidhiwa kwa watendaji Kata hivyo wasimamie ugawaji huo kwa wananchi na pia kusimamia maendeleo yake.
Amesema mwakani tutaongeza miche zaidi ya mara tatu ya mwaka huu ili wananchi wawe na maisha mazuri kwa kujenga nyumba nzuri,wasomeshe watoto na pia kukidhi garama za matatibabu pale wanapougua. Pia amewaasa viongozi na Waheshimiwa madiwani kuw wakirudi katika maeneo yao wawahamasishe wananchi kuwa miche ya mikorosho ipo hata kwa kuknunua waweze kupanda kwa wingi ili waondokane na hali duni ya kipato.
Pia Ofisa Kilimo,Uvuvi na Umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.Yibarila Chiza ameelezea mikakati ya kuendeleza kilimo cha Korosho kwa kusema kuwa Halmashuri imelenga kuongeza maeneo ya uzalishaji wa zao la korosho katika msimu wa mwaka 2018/2019 kiasi cha ekari laki moja kutarajiwa kupandwa miche ya mikorosho ambayo ni mara tatu ya msimu huu.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa