Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya semina ya Uelewa wa fedha za ruzuku ya maendeleo iliyoboreshwa (LGDG) na mfumo wa Fursa na Vikwazo ulioboreshwa (IMPROVED O&OD) kwa Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Semina iliendeshwa na wataalamu wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ililenga kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu fedha za ruzuku ya manendeleo iliyoboreshwa katika maeneo ya:-.
1.Maana na umuhimu wa LGDG
2. Matokeo ya LGDG iliyoboreshwa
3. Changamoto za LGDG iliyopita
4. Vigezo 9 vya kiutendaji na vigezo vya msingi
5. Mgawanyo wa fedha za LDGD
6. Matumizi ya fedha za LDGD
Kwa upande wa ugatuaji wa madaraka (D by D), umuhimu wa mfumo wa fursa na vikwazo ulioboreshwa katika maeneo ya:-
1. Maana ya mpango wa fursa na vikwazo ulioboreshwa (O&OD)
2. Maana ya jitihada za jamii na aina zake
3. Mantiki ya Halmashauri kusaidia jitihada za jamii kwa kuangalia Uhalisia wa Tanzania ndani ya Serikali za Mitaa na Faida za kutoa usaidizi kwa jitihada za jamii.
4. Vigezo vya kuchambua jitihada za jamii
5. Aina za usaidizi wa jitihada za jamii
6. Mifano halisi ya jitihada za zamii kwa video.
Akifungua semina hiyo Jana, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alipongeza ushirikishaji wananchi kutoka ngazi za chini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati na miradi ya maendeleo iliyokamilika kwa kuwepo na nia ya dhati kwa wananchi
Diwani Kata ya Kwamatuku Mh. Mustafa Beleko akiuliza swali la ufafanuzi.
Viongozi wakisikiliza kwa makini
Wataalmu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga
Waheshimiwa Madiwani na wakuu wa Idara na Vitengo kwenye ukumbi wa Halmashauri
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa