Wananchi Wilayani Handeni wameaswa kupanda miti kwa wingi hususani ya kibiashara ili kujikwamua kiuchumi badala ya kuvuna miti kwaajili ya uchomaji mkaa na mbao.Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya Bw. John Mahali alipokuwa akifungua zoezi la upandaji miti lililofanyika Kiwilaya Kijiji cha Kwamkunga Kata ya Komkonga.Ufunguzi huo ulijumuisha viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji, waheshimiwa madiwani , wataalamu mbalimbali wa Halmashauri na Wananchi ambapo miti 6500 na mikorosho 800 imepandwa maeneo mbalimbali ya Wilaya.
kwa maelezo zaidi soma hapa
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa