Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao kazi na taasisi zisizo za Kiserikali zinazofanya kazi zake kwenye Halmashauri ya Handeni.
Taasisi hizo ni pamoja na AMREF, CAMFED, Hope 4 young girls, NALIDO, CDRP, Tree of Hope na INUKA. Mashirika mengine ni AFRIWAG, Room to Read, DORCAS, NUMAWATA na NACONGO Mkoa wa Tanga.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Rachel Mbelwa kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni.
Lengo la kikao hicho ni kuwasilisha taarifa za mashirika hayo kuhusu mafanikio, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto kushirikiana na Halmashauri ya Handeni.
Pia namna taasisi hizo zitakavyoweza kusaidia wananchi wa Msomera kwa ujenzi wa nyumba za watumishi, kutoa elimu ya ujasiliamali kwa makundi lengwa ya wanawake, wazee na watu wenye mahitaji maalum na uboreshaji wa huduma za jamii.
Taasisi hizo zote kwa pamoja wameazimia tarehe 30 Machi 2023 kutembelea Kijiji cha Msomera ili kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi.
Bi. Rechel Mbelwa, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halamshauri ya Handeni, akitoa maelekezo kwenye kikao hicho.
Viongozi wa taasisi za Kiraia wakimsikiliza mwenyekiti wa kikao hicho.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa