Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. Kanansia Shoo ameongoza kikao maalumu cha MAAFA ili kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na kutoa huduma kwenye matukio ya dharula kama vile magonjwa ya mlipuko, ajali, mafuriko, tetemeko la Ardhi.
Katika Kikao hicho kilichohusisha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya kwa ngazi ya Halmashauri( CHMT).
Kikao kimeazimia wataalam wa afya kutoka ofisini na kwenda kutoa elimu kwa jamii ili kujikinga na magonjwa ya milipuko na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea katika jamii.
Elimu hiyo ianze kutolewa kwenye mikusanyiko ya watu ambayo ni kwenye shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, maeneo ya kutolea huduma za afya, kwenye masoko pamoja na maeneo ya ibada.
Aidha ili kuepukana ana magojwa ya mlipuko jamii inatakiwa kufanya usafi kwenye maeneo yao hasa kusafisha mifereji ya maji taka, kufukia mashimo, kuhakikisha utunzaji mzuri wa chakula pamoja na watoto wa wadogo wanapata mlo kamili.
Aidha katika kikao hicho wataam hao wametakiwa kuwaambia wananchi kuwa kama kuna mtu yoyote akiona dalili za kuumwa ugonjwa wowote katika mazingira yao wanayoishi anatakiwa kufikishwa kwa haraka kwenye eneo la kutolea huduma ya afya ili kupata matibatu mapema kabla hajazidiwa.
Dkt. Kanansia Shoo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa