Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Mazao (TARI) tawi la Naliendele kilichopo Mtwara kimetoa elimu kwa wataalam wa kilimo wa Halmashauri na wakulima namna ya kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa kwenye zao la korosho.
Mkuu wa idara ya kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmshauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Yibalila Kamele Chiza amesema kwa miaka mitatu sasa Halmashauri imetekeleza maagizo ya Serikali ya kila Halmashauri kulima korosho na imewekeza kwenye zao la korosho kama zao la kimkakati na kuwapatia wakulima wa zao la korosho miche bure bila malipo yoyote kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele kilichopo Mtwara.
Bw. Chiza amesema msimu wa kwanza wa mavuno ya korosho umewadia ni muda muafaka kama Halmashauri kuwapatia mafunzo wataalam na wakulima watakoenda kusaidiana na wakulima wenzao kupulizia dawa kwenye zao la korosho ili kuuwa wadudu waharibifu na kupata mazao yaliyo bora.
Mtafiti wa zao la Korosho kutoka TARI tawi la Naliendele Bw. Dadili Majune amesema wao kama wataalam wanaendelea kutoa elimu ya magojwa kwenye zao la korosho na ameyataja magonjwa makuu yanayoshabulia zao la korosho ambayo ni Ubwiri Unga, Braiti na debeji.
Baada ya kupata elimu wataalam wameweza kutambua dalili za magonjwa hayo na namna ya kudhibiti magonjwa hayo ili kuleta tija kwenye uzalishaji wa zao la korosho.
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Bw. Yibelila Kamele Chiza (katikati) wa Halmashauri ya Handeni akitoa maelekezo kwa wataam wa kilimo.
Mtafiti wa zao la Korosho kutoka TARI tawi la Naliendele Bw. Dadili Majune, aliyeshika fimbo akitoa ufafanuzi wa magonjwa ya zoa la korosho kwa wataalam wa Halmshauri.
Wataalam wa kilimo kutoka Halmashauri ya Handeni, wakimsikiliza Mtafiti kutoka TARI tawi la Naliendele.
Mtaalam akipulizia dawa kweye zao la korosho.
Wataalam wa kilimo pamoja na wakulima, wakiangalia wadudu waaribifu kwenye zao la korosho.
Korosho zikiwa bado hazijakomaa.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa