Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen ameogonza Halmashauri hiyo kukabidhi vyumba 91 vya madarasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19 kwa shule za Sekondari na shule shikizi vilivyokamilika kwa asilimia 100% .
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wananchi wanyonge kwa vitendo kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Handeni fedha kwaajili ya ujenzi wa Madarasa ambayo yatamaliza uhaba wa madarasa na kuondoa mrundikano wa wanafunzi darasani.
Pia Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mkurugenzi kuhakikisha shule zote shikizi za Msingi zinasajiliwa haraka ili shule zitakapofunguliwa wanafunzi wa darasa la kwanza waanze kusoma kwenye shule hizo.
Kwakumalizia Mhe. Mchembe ametoa maagizo kuwa shule zitakapofunguliwa wanafunzi wote waliofaulu wanatakiwa kwenda kuripoti kwenye shule zao walizopangiwa na kama kuna wazazi wamewapeleka watoto zao kufanya kazi za ndani watawakamata wazazi na katoa maagizo kuwa watendaji na wenyeviti wote wafuatilie wanafunzi wanotakiwa kwenda shuleni waende shule.
Akisoma taarifa ya Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Bw. Saitoti Zelothe Stephen amesema wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wanampongeza Rais wa awanu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta jumla ya kiasi cha Shilingi bilioni mbili na milioni miambili za UVIKO-19 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa 72 kwa shule za Sekondari na shule shikizi 7 za Msingi pamoja na miundombinu ya afya ya jengo la Huduma za dharura na nyumba ya mtumishi wa Afya. Amesema utekelezaji wa miradi hii ulitumia njia ya (FORCE ACCOUNT) na kuweza kuokoa kiasi cha shilingi 89,024,420.50
Bw. Saitoti alisema ujenzi huu umemaliza uhaba wa vyumba vya madarasa ambao wangepata wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza na darasa la kwanza kwa mwaka 2022, ambapo amesema kwa mwaka 2022 wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 5,717 kati yao wasichana 3,024 na wavulana 2,693. Aidha amesema kati ya shule shikizi 7 zilizoletewa fedha za UVIKO19 shule 4 zinafanyiwa utaratibu wa kupata usajili ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu, shule hizo ni Kwemigunga, Kwachiti, Tengwe na Kwambalu.
Alihitimisha kwa kusema kuwa fedha za miradi hiyo imesaidia pia kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kupata ajira za muda za ujenzi kwani waliweza kuajiriwa watu 819 lakini pia mama ntilie waliokuwa wanauza vyakula na vinywaji kwa wafanayakazi waliweza kujipatia kipato.
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe, akitoa maelekezo ya Wilaya kuhusu majengo ya madarasa yatokanayo na fedha za UVIKO-19
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen akisoma taarifa ya madarasa ya UVIKO-19 mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wiliaya ya Handeni.
Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Handeni wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya wakati wa makabidhiano ya Madarasa ya UVIKO-19.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye makabidhiano ya madarasa ya UVIKO-19.
Madarasa ya Shule ya Sekondari ya Martine Shigele yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa