TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William M. Makufwe anawatangazia wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuwa Halmashauri imenunua mbegu za Korosho inayoweza kuzalisha miche 600,000 kutoka Kituo cha Utafiti Nalielendele iliyoko Mkoa Mtwara.
Hivyo anawataarifu wananchi wote wenye mahitaji ya kupanda Korosho wajiandikishe kwenye ofisi za Kata au vijiji wakiainisha mahali lilipo shamba na ukubwa wake
Aidha amesema Wakulima watapewa miche/mbegu hiyo kwa masharti yafuatayo
Mbegu/ miche hiyo itaanza kugawiwa bure kwa wakilima kuanzia tarehe 15-02-2019 katika Ofisi za Makao makuu ya Kata . Hivyo wakulima wanahimizwa kujiandikisha mapema kiasi cha miche/ mbegu wanayohitaji.
Ikumbukwe kuwa ekari moja kitaalamu inauwezo wa kupandwa miche 30.
Nawatakia utekelezaji mwema.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na mahusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa