*Kazi Imeanza*
Wananchi wa Kijiji cha Kabuku nje wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando wameshiriki zoezi la uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa madarasa 7 katika shule ya Msingi Kabuku Nje umekamilika.
Serikali Kupitia mradi wa BOOST imeipatia Shule ya Msingi Kabuku Nje kiasi cha Milioni Miamoja themanini na saba *(187,000,000)* kwaajili ya ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa na vyoo matundu 6.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia kiasi cha Shilingi 1,527,000,000 kwa ajili ya vyumba 53 vya madarasa na vyoo matundu 150.
Handeni tunasema
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa