HANDENI VIJIJINI IMEFANYA BARAZA LA ROBO YA NNE YA MWAKA 2020/2021.
Baraza hilo la madiwani lilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Katika baraza hilo waheshimiwa madiwani walisoma taarifa za Kata kwa sekta za elimu, afya, kimo, mifugo, michezo na utawala bora zikionyesha mafanikio, changamoto na utatuzi wa changamoto.
Pia sekta ya barabara (TARURA) na maji (RUWASA) walitoa taarifa za utekelezaji wa shughuli zao na wajumbe wakaomba hizo sekta kufanya upembuzi yakinifu wa maeneo mbalimbali ili kutatua kero za barabara na maji kwa kuwa maeneo mengi yana changamoto ya huduma hizo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Bw.Mashaka Boniphace Mgeta alimpongeza Mkurugenzi kwa kuteuliwa na kumkaribisha Handeni.
Aidha amewasihi waheshimiwa madiwani na watumishi kumpa ushirikiano Mkurugenzi huyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe amewasihi waheshimiwa Madiwani kumpa ushirikiano ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Handeni na anasema maendeleo hayo yanahitaji mapato hivyo amewasihi washirikiane katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.
"Kabla ya kuja kushikana mashati kuhitaji zahanati na madarasa nawaomba Mwenyekiti pamoja waheshimiwa tujumuike kwa pamoja katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato" alisema Zelothe.
Katibu Tawala Wilaya ya Handeni Bw Mashaka Boniphace Mgeta akizungumza na wajumbe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw Saitoti Zelothe akiongea katika baraza hilo.
Viongozi(kulia ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni, kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya na Katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Handeni) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao.
Wajumbe wakifuatilia kikao
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa