Idara ya elimu kupitia kitengo cha Sayansikimu iliadhimisha Kilele cha maadhimisho ya Juma la kunawa mikono na usafi wa mazingira katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkomba Kata ya Kwachaga, Kijiji cha Mkomba ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Tawala Wilaya ya Handeni Bi Upendo Mgeta ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kunawa mikono,usafi wa mazingira na umuhimu wa vyoo ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ukiwepo gonjwa hatari la UVIKO 19.
Akizungumza Afisa Tawala wa Wilaya wa Wilaya ya Handeni Bi.Upendo Magashi alipongeza ufanyikaji wa maadhimisho hayo ili wananchi wachukue tahadhari ya magonjwa ya mlipuko na kuambukiza kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Naye Afisa Sayansikimu Bi Grace Mbanga aliwashukuru wadau mbalimbali wakiwepo shirika la Amref, World vision, Dorcas na Hope for young girls kwa kujitokeza kusaidia ufanyikaji wa maadhimisho hayo lakini pia wamekuwa wakichangia katika ujenzi wa vyoo shuleni kitu kitakachosaidia kupunguza kuzuia kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko.
Katika maadhimisho hayo zilitolewa zawadi za ndoo za kunawia,fyekeo,jembe, jagi la kumwagilia kwa shule zilizofanya vizuri katika usafi wa mazingira ambapo shule hizo ni Shule za msingi Nyasa, kwamatuku na Madebe na kwa upande wa Shule za Sekondari ni St. Wilbada, Segera na Kang'ata.
Sabamba na hilo pia mgeni rasmi alitoa vyeti kwa wadau kama ishara ya kutambua mchango wao katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Afisa Tawala wa Wilaya wa Wilaya ya Handeni Bi.Upendo Magashi akikabidhi zawadi ya jagi la kumwagilia maji.
Afisa Tawala wa Wilaya wa Wilaya ya Handeni Bi.Upendo Magashi, wapili kutoka kushoto akiwa na maafisa kutoka Halmashauri ya Handeni kabla ya maadhimisho hayo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa