Siku ya UKIMWI duniani huadhimishwa 1 Desemba kila mwaka ili kueneza ufahamu wa ugonjwa wa UKIMWI unaosababishwa na uambukizi wa Virusi vya UKIMWI ni kawaida kuwa na ukumbusho huo siku hii ili kuwajali watu ambao wamefariki kutokana na ugonjwa wa UKIMWI. Kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI inasema “zingatia usawa tokomeza UKIMWI, tokomeza magonjwa ya Mlipuko”
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imeadhimisha siku ya UKIMWI duniani kwenye viwanja vya Tuliani vilivyopo kata ya Kwachaga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo amesema kaulimbiu ya Mwaka huu ya kuzingatia usawa na tokomeza UKIMWI iendane sambamba na wanaume wajitoleze kwa wingi kwenda kupima ili watambue afya zao.
Kwakutambua watoto wa kike namna wanavyorubuniwa na kuambukizwa ugonjwa wa UKIMWI, Mhe. Mchembe amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni kuandaa mikakati ya ujenzi wa hosteli kwenye shule za sekondari ili wanafunzi wa kike wasitembee umbali mrefu.
Pia Mkuu wa Wilaya Mhe. Mchembe aliwaongoza wananchi wa kwachaga kupima ugonjwa wa UKIMWI ili kutambua afya zao.
Kwenye maadhimisho hayo huduma mbalimbali zilitolewa kama vile upimaji wa Virusi vya UKIMWI (VVU), chanjo ya Ugonjwa wa UVIKO-19, elimu ya lishe na magonjwa sugu yasiyoambukiza na upimaji wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB). Huduma nyingine ni pamoja na utolewaji wav yeti vya kuzaliwa kwa watoto waliopo chini ya miaka mitano, uandikishaji wa bima ya afya iliyoboreshwa (iCHF) na elimu ya ukatili wa Kijinsia.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe (katikati) akitolewa damu kwaajili ya kupimwa virusi vya UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen, akiwaasa na kuwasisitiza vijana kuacha tamaa ambazo zitawapelekea kupata ugonjwa wa UKIMWI.
Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Jogia Mjankwi kulia akitoa cheti cha kuzaliwa cha mtoto chini ya miaka mitano kwa mzazi.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa