Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao cha baraza la wafanyakazi Ili kupitia mpango wa rasimu ya bajeti ya Halmashauri ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwatetea wananchi hivyo watanzania na wafanyakazi wote kwaujumla wazidi kumuombea Rais Afya njema Ili wazidi kuuona upendo wake kwa wafanyakazi.
Bw. Saitoti amesema kuwa baraza hilo ni muhimu kupitia rasimu hiyo ya bajeti ili kuboresha kabla ya kwenda kujadiliwa kwenye baraza la madiwani pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Walimu kwa kusimamia Miradi ya Ujenzi wa miundombinu ya Madarasa ya UVIKO-19 na Miradi yote inayotekelezwa kwenye shule zao.
Kwakumalizia Bw. Saitoti amewaasa watumishi kusimamia uadilifu na uaminifu kwenye mazingira yao ya Kazi.
Kwaupande wa viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wameishauri Serikali kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya Kazi vizuri na wameomba kuboreshewa maslahi pamoja na mazingira bora ya kufanyia Kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen (Aliyevaa tai), akiongea kwenye kiako Cha baraza hilo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini rasimu ya bajeti ya Halmashauri.
Watumishi mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa