Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Mussa Mwanyumbu ameongoza kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri, Ujenzi wa nyumba ya Mganga mkuu wa Halmashauri, Ujenzi wa jengo la uthibiti ubora wa Elimu na shule ya sekondari ya Martin Shigela iliyoko kijiji cha Mzeri kata ya Misima. Miradi mingine ni Shule za sekondari Segera na Kabuku na kiwanda cha kuchakata muhogo cha Jipe Moyo kilichopo kata ya kitumbi.
Wakati ya ziara hiyo mwenyekiti Mh. Mwanyumbu amempongeza Mkurugenzi wa Halmashuri na watumishi kwa kusimamia miradi hiyo kwa ukamilifu.
Aidha, kamati hiyo ya fedha, uchumi na mipango imeshauri Halmashauri kuchimba kisima cha maji katika eneo la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ili kurahisisha upatikanaji wa maji ya uhakika kwenye ujenzi huo na kuepuka gharama za ununuaji wa maji.
Kwaupande wa Afisa mipango wa Halmashauri ya Handeni Bi. Edina Katalaiya kwaniaba ya Mkurugenzi ameishukuru kamati ya fedha, uchumi na mipango kufanya ziara ili kujionea miradi inayotekelezwa na Halmashauri.
Bi Edina Katalaiya amesema kuwa Halmashauri itapeleka mabati 162 na saruji mifuko 90 kwenye ujenzi wa shule ya Sekondari Kabuku, na mifuko 100 ya saruji kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya Martin Shigela iliyopo Misima.
Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha, uchumi na mipango Mhe. Mussa Mwanyumbu wapili kushoto, akimsikiliza Mhandisi John Mshahara kulia walipotembelea ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri.
Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ilipofika kukagua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Jipe Moyo kilichopo kata ya Kitumbi.
Afisa mipango wa Halmashauri Bi.Edina Katalaiya aliyeshika kitabu, akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Martin Shigela iliyopo Kata ya Misima.
Mhandisi John Mshahara wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wapili kushoto, akitoa ufafanuzi kwa kamati ilipotembelea ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri.
Muonekano wa Jengo la makao makuu ya Halmashauri hatua lililofikia ujenzi bado unaendelea.
Jengo la Uthibiti ubora wa Elimu Halmashauri Wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa