Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango(FUM) kwa kuambatana na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wamefanya ziara ya ukaguzi wa miaradi ya maendeleo kwa lengo la kujua hali halisi ya miradi , mahali ilipofikia na thamani ya pesa iliyotumika ( value for money).
Maeneo yaliyotembelewa na Kamati ya FUM ni pamoja na mgodi wa madini wa magambazi, maabara ya shule ya Sekondari Kwaluguru,jingo la upasuaji lililopo kwenye kituo cha afya cha Mkata na ujenzi wa bweni la wavulana shule ya sekondari Kisaza.
Katika ziara hiyo Waheshimiwa madiwani wamefanikiwa kupata maelezo ya lini mgodi wa magambazi utaanza kufanya kazi rasmi na namna ambavyo wameshirikisha jamii na wataendelea kushirikisha jamii kwa kutoa ajira zinazoweza kufanywa na wazawa wa eneo hilo,kushiriki katika shughuli za kijamii zinazowagusa moja kwa moja wananchi na utoaji wa kodi kwa Serikali kuu na Halmashauri.
Kamati imeagiza pia miradi ambayo imechukua muda mrefu kukamilika, iweze kukamilika kwa wakati ili wanufaika wa miradi hiyo waweze kupata huduma bora kwa wakati unaostahili.
Aidha Kamati imepongeza ujenzi wa jengo la upasuaji lililopo katika kituo cha afya cha Mkata kwa namna ambavyo thamamni ya fedha imeonekana wazi katika ujenzi wa jengo hilo na uwepo wa baadhi ya vifaa vinavyohitajika.
Kwenye miradi ambayo wananchi wanapaswa kushiriki nguvu kazi Kamati imeagiza viongozi wa Kata na maeneo husika kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki nguvu kazi ambazo wanazoweza kufanya ili kusaidia ukamilishwaji wa miradi kwa wakati, hasa ukizingatia miradi hiyo ni kwaajili ya manufaa yao na jamii nzima inayozunguka eneo husika hivyo, wanaowajibu kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kuumiliki mradi uliopo kwenye maeneo yao ili uweze kutunzwa vyema na wananchi wenyewe.
Kamati ikipata maelezo mafupi namna mtambo unavyochakata mchanga hadi upatikanaji wa dhahabu Magambaz.
Mtambo wa kuchakata mchanga hadi hatua ya kupatikana dhahabu.
Eneo ambalo CANACO Wataendelea kuchimba kuelekea mlimani ili kupata dhahabu.
Kamati ikipata maelezo kutoka kwa msemaji wa CANACO juu ya matumizi ya mitambo inayotumika kulainisha mawe ili wapate dhahabu.
Kamati ikipata maelezo mafupi juu ya jengo hilo.
Kamati ikitoka kwenye jengo la upasuaji kituo cha afya Mkata.
Kamati ya FUM na wataalamu mbalimbali wakiwa kwenye jengo la bweni la wavulana shule ya sekondari Kisaza.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa